Monday, March 28, 2016

SABABU ZA DIAMOND PLUTNUMZ KUANZISHA WCB






Tasnia ya muziki nchini inazidi kupiga hatua kila siku na hii inatokana na jitihada zinazofanywa na wanamuziki wenyewe kwakuwa na dhamira ya kweli ya kutoboa kimataifa, muziki wa Tanzania kwasasa unatambulika ulimwenguni tofauti na zamani.DIAMOND PETER SQUARE

Tunaweza kuwa mashahidi wakubwa kwasababu wasanii wetu wamekuwa wakipata mialiko mbalimbali nje ya nchi na hii ni ishara kuwa muziki wetu unatambulika katika nchi hizo,licha ya kupiga hatua hizo baadhi ya wasanii wakubwa hawajaishia hapo wameamua kuanzisha vikundi vya wasanii ili kukuza vipaji vya wasanii wachanga kufikia anga za kimataifa.mama15-marquee-diamond-800x451

Nitazungumzia moja ya kundi linalo fanya vyema kwa sasa kutokana na ufanisi wa kazi zao ni Wasafi Classic Baby (WCB) kundi ambalo limeanzishwa na mwanamuziki icon wa Tanzania Diamond Plutnumz chini ya usimamizi mahiri wa mameneja watatu Babu Tale, Salaam SK na Said Fella.DIAMOND NA MAMENEJA WAKE

Unaweza ukawa na swali ambalo linagonga kichwa chako kwanini Diamond ameamua kuanzisha WCB, hivi karibuni staa huyo alisikika katika vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini akieleza kuwa moja ya sababu za kuanzisha kundi hilo ni kuibua vipaji vipya ambavyo vitaweza kupeperusha vyema bendera ya nchi na kuleta tuzo mbalimbali za kimataifa.raymond wcb

Pia staa huyo alisisitiza kuwa WCB ina wasanii wawili mpaka sasa ambao ni Raymond hit maker wa Kwetu na Harmonize anaetamba na wimbo wake wa Bado, ila lengo ni kuwa na wasanii watano pekee ambao wataweza kuwamudu, kalamu ya mtembezi inahitimsha kwa kueleza kuwa ni vyema wasanii mbalimbali wakaiga mfano wa Diamond Plutnumz ili kuibua vipaji vipya vyenya ladha tofauti katika mziki wa Tanzania na kuutangaza zaidi.harmonize and diamond


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment