Tuesday, March 29, 2016

Mwanzo wa kuangamizwa magaidi wa ISIS baada ya kukombolewa Palmyra , Syria



Mwanzo wa kuangamizwa magaidi wa ISIS baada ya kukombolewa Palmyra , Syria
Mafanikio ya kistratijia ya Jeshi la Syria katika kuukomboa kikamilifu mji wa kihistoria wa Tadmur au Palmyra ni jambo ambalo limezidi kumuimarisha Rais Bashar al Assad mbali na kuwa ni ujumbe kwa dunia kuwa, jeshi la Syria ndilo pekee linaloweza kuangamiza magaidi wa ISIS au Daesh nchini humo.
Kamandi Kuu ya Jeshi la Syria imetangaza kuwa, kikosi maalumu cha askari wa jeshi la nchi hiyo mashariki mwa mkoa wa Homs kwa kushirikiana na wananchi waliojitolea kupigana na pia kwa msaada wa Jeshi la Russia, siku ya Jumapili walifanikiwa kuchukua udhibiti kamili wa mji wa Tadmur. Mji huo ulikaliwa kwa mabavu na magaidi wa ISIS mwezi Juni mwaka 2015.
Hatua ya jeshi la Syria kuukomboa mji wa Tadmur ina umuhimu wa kistratijia kwani mji huo ni kiunganishi baina ya maeneo ya kati, kusini, mashariki na kaskazini mwa Syria.
Aidha kwa mtazamo wa kiuchumi, mji mkongwe wa Tadmur una visima vya mafuta, gesi na madini na hivyo ni nguzo muhimu ya uchumi wa Syria. Ushindi wa jeshi la Syria katika mji wa Tadmur, ambao kwa Kiingereza ni maarufu kama Palmyra, ni pigo kubwa sana kwa magaidi wa ISIS.
Mji huo ulikaliwa kwa mabavu wakati muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani dhidi ya ISIS ukiwa umeshaanza hujuma Syria. Mji huo aidha umekombolewa pasina kuhusika muungano huo wa Marekani.
Kama alivyosema Rais Bashar al Assad wa Syria, kukombolewa mji wa kihistoria na kistratijia wa Tadmur ni ishara kuwa Jeshi la Syria limefanikiwa katika vita dhidi ya ugaidi na kwamba muungano wa kijeshi unaongozwa na Marekani na unaojumuisha nchi 60 haulipi uzito suala la vita dhidi ya ugaidi.
Mafanikio muhimu ya jeshi la Syria katika kuwatimua magaidi wa ISIS huko Palmyra, ni mwanzo wa kuangamizwa kundi hilo la magaidi wakufurishaji. Kudhibitiwa mji huo ni hatua muhimu katika oparesheni zaidi dhidi ya ISIS katika miji muhimu ya Deir Ezzor, Al-Hasakah na Ar Raqqah.
Kukombolewa mji wa Tadmur ni tukio lenye taathira hasi wa ISIS nchini Syria na Iraq.
Ushindi wa Jeshi la Syria huko Tadmur pia utapelekea Rais Bashar al Assad kuwa na nafasi kubwa ya kidiplomasia katika utatuzi wa mgogoro wa Syria. Rais Assad ameimarika katika uga wa kidiplomasia na kijeshi na hivyo atakuwa na nafasi muhimu na kwa msingi huo kuzungumza naye ni jambo la lazima.
Madola ya magharibi hayana budi ila kufanya mazungumzo na Bashar al Assad kuangamiza magaidi na kuwazuia kufika Ulaya, hii ni kwa sababu hivi sasa magaidi wa ISIS wanahesabiwa kuwa adui nambari moja wa nchi za Ulaya.
Kwa kuzingatia hujuma ya hivi karibuni ya ISIS mjini Brussels ambao ni kitovu cha Umoja wa Ulaya, ni wazi kuwa magaidi hao wamepenya katika miji wa Ulaya. Njia pekee ya kuzuia kuenea ISIS ni kumuunga mkono Bashar al Assad katika kuangamiza magaidi wa ISIS Syria na Iraq.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment