Maelfu ya wakimbizi wa Mali waliokimbilia katika nchi jirani ya Burkina Faso wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwa sasa wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) yamesema katika taarifa zao kwamba, zaidi ya wakimbizi 31 elfu wa Mali waliokimbia machafuko katika nchi yao na kuomba hifadhi nchini Burkina Faso wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. Ripoti ya WFP na UNHCR imeeleza kwamba, hali ya wakimbizi hao kwa upande wa chakula ni mbaya na kwambo wanakabiliwa na baa kubwa la njaa.
Imeelezwa kuwa, hali ya wakimbizi hao katika miezi mitatu ijayo itakuwa mbaya mno.
WFP na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR yametahadharisha kwamba, endapo hakutachukuliwa hatua za maana na za haraka, basi wakimbizi hao watakumbwa na maafa makubwa.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lilitangaza kuwa, idadi ya wakimbizi raia wa Mali wanaokimbilia nchini Niger imeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
No comments:
Post a Comment