Imeelezwa kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itafanyika katika muda muafaka kufuatia kufikiwa makubaliano kati ya pande mbili na ili kuwezesha kufanyika uratibu zaidi.
Kabla ya hapo ilikuwa imetangazwa kuwa, safari ya Rais HassanRouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Austria ingefanyika tarehe 30 na 31 za mwezi huu, hata hivyo ziara hiyo itafanyika katika muda muafaka ili kudhamini mazingira mazuri zaidi kuhusu mpango na makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi mbili hizo kwa uratibu wa nchi mwenyeji.
Itakumbukwa kuwa Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo Jumatano tarehe 30 Machi alitarajiwa kuelekea Vienna Austria kujibu mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Heinz Fischer. Wakati huo huo Rais wa Austria amesema amesikitishwa na kuakhirishwa safari ya Rais wa Iran nchini humo na kubainisha kuwa ni jambo la kawaida kwa serikali yoyote kuchukua uamuzi kuhusu usalama wa kiongozi wake wa ngazi ya juu.
No comments:
Post a Comment