Showing posts with label TANZIA. Show all posts
Showing posts with label TANZIA. Show all posts

Monday, August 8, 2016

Mama Mwenye VVU Pamoja na mtoto wake wakutwa wamekufa mlimani MKAZI wa wilayani Chato


MKAZI wa wilayani Chato mkoani Geita, Rose Joseph (32) aliyekuwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na mtoto wake mwenye umri wa miaka kati ya minne na mitano, wamekutwa mlimani wakiwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Nafuba kilichoko ndani ya Ziwa Victoria wilayani Bunda mkoani Mara.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Nafuba, Zakaria Kachimu alisema tukio hilo liligundulika juzi saa 9:00 mchana katika eneo la mlima huo, baada ya wananchi waliopita katika eneo hilo kuona kwanza mwili wa mwanamke huyo.

Alisema baadaye wananchi walifanikiwa kumtafuta mtoto wake na kumkuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine. 

Kachimu alisema mwanamke huyo alifika kisiwani hapo Julai 25, mwaka huu, akiwa na mtoto mdogo wa kiume aitwaye Kababu, akiwa anatafuta kazi ya kuhudumia kwenye mgahawa.

Alisema kuwa kulingana na afya ya mwanamke huyo kudhoofika, kila sehemu alikokwenda kutafuta ajira hiyo alikataliwa. Baada ya kukosa ajira hiyo mwanamke huyo alikwenda kwa jamaa yake ambaye pia ni mwanamke aliyeko kisiwani hapo na kuishi nyumbani hapo.

Baadaye mwanamke huyo alikwenda kutibiwa katika zahanati moja iliyoko kisiwani hapo na ikagundulika kuwa ana mambukizi ya virusi vya Ukimwi na kuambiwa aende katika Kituo cha Afya Kisorya kwa ajili ya kujiunga kwa kupewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs).

Hata hivyo ilielezwa kuwa mwanamke huyo hakwenda kwenye kituo hicho kama alivyoshauriwa na mganga wa zahanati hiyo.

Aidha, Ofisa Mtendaji huyo alisema siku ya tukio wananchi waliopita katika eneo hilo walikuta mwili wa mwanamke huyo katika mlima huo na kuamua kutoa taarifa, ambapo tena walianza kutafuta mtoto wake na kukuta pia akiwa amekufa katika eneo lingine.

Alisema kuwa chanzo cha vifo hivyo ni cha kutatanisha na kwamba huenda mtoto huyo alikufa kwa njaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’anzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema upelelezi unafanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.

Wednesday, May 11, 2016

Mwanafunzi Askari Chuo cha Anga cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Ajiua Kwa Kujipiga Risasi


Mwanafunzi wa Chuo cha Anga (Skua) cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Kange jijini Tanga, Philip Fred (28) amejiua kwa kujipiga risasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kwamba tukio hilo ni la jana saa 1.15 usiku katika chuo hicho kilichopo kata ya Maweni nje kidogo ya jiji.

Alisema askari mwenye cheo cha Koplo mwenye namba MT 81627 alijiua wakati akiwa katika eneo la lindo chuoni hapo.

“Kimsingi chanzo cha kifo cha askari jeshi huyo bado hakijajulikana na imefahamika kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa ‘Level one’ chuoni hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo”,alisema Kamanda.

Katika tukio jingine Kamanda alisema askari wanamshikilia mkazi wa mtaa wa Mgwisha, kata ya Pongwe jijini Tanga, Masudi Hamis (22) kwa tuhuma za kukutwa na sare moja ya askari wa JWTZ.

Sunday, April 24, 2016

Mwanamuziki Papa Wemba ameaga dunia

Image captionPapa Wemba ameaga dunia
Nyota wa muziki wa Soukous ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- Papa Wemba amefariki dunia
Papa Wemba ambaye jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, alianguka na kufa jukwaani akiwatumbuiza maelfu kwa maelfu ya mashabiki wake waliojitokeza katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Alikuwa maarufu katika micharazo ya muziki wa Soukous,
Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki maarufu sana barani Afrika na kote duniani.
Image captionPapa Wemba alianguka katika tamasha la muziki mjini Abidjan Ivory Coast.
Msanii huyo nguli mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni anasemekana alianza kutetemeka, kisha akaanguka na kuzirai, alipokuwa akitumbuiza jukwaani Abidjan.
Papa Wemba, kama alivyofahamika na mashabiki wake, alikuwa na umri wa miaka 66 na alikuwa amepata uraia wa Ubelgiji.
Vibao vyake ni kama Mwasi,show me the way, Yolele, Mama,Proclamation"Chouchouna" (Papa Wemba), "Eluzam" na " Mbeya Mbeya" (Evoloko Lay Lay), "BP ya Munu" (Efonge Gina), "Mwana Wabi" , "Mizou" (Bimi Ombale) , "Zania" (Mavuela Somo.

Saturday, April 9, 2016

Muimbaji maarufu afariki jukwaani

Image captionMuimbaji maarufu afariki jukwaani
Huzuni na mshangao umeghubika Indonesia baada ya muimbaji maarufu Irma Bule, aliyekuwa akiwatumbuiza mashabiki wake kuanguka na kufariki dunia jukwaani
Yamkini bi Bule aliumwa na nyoka yapata dakika 45 zilizotangulia katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Java Indonesia.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.
Japo nyoka huyo alikuwa ameng'olewa chonge zake , kwa njia moja au nyingine aliweza kum'gata na kuingiza sumu ndani ya damu yake.
Duru zinasema kuwa alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.
Aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang'amua hali haikuwa nzuri.
Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.
Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.

Msanii wa Muziki wa dansi Ndanda Kosovo Afariki Dunia



Msanii wa muziki wa dansi Ndanda Kosovo amefariki dunia asubuhi ya leo katika hosptali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwanamuziki mwenzake Kardinal Gento, Ndanda alikuwa alisumbuliwa na matatizo ya vidonda vya tumbo, maradhi yaliyopelekea kulazwa katika hospitali ya Mwananyamala Dar es salaam.

Kardinali ambaye pia ni mjomba wake, amesema kuwa Ndanda alihamishiwa katika Hosptali ya Taifa Muhimbili siku mbili zilizopita kutoka Mwananyamala baada ya tatizo lake kushindikana kabla ya mauti kumkuta majira ya saa mbili asubuhi ya leo.

"Nilikuwa naye hospitali tangu jana, na nimekesha naye, ilipofika asubuhi hali yake ilikuwa nafuu, nikaondoka kurudi nyumbani kwa ajili ya chakula, nikaacha anafanyiwa mpango wa damu maana alikuwa amepungukiwa damu, lakini muda mfupi baada ya kuondoka hospitali hapo nikapigiwa simu kuwa Ndanda amefariki, ilikuwa mida ya saa 2 asubuhi” Amesema Gento.

Gento amesema taratibu za mazishi zinasubiri mama yake arudi Dar es salaam, ndipo wataamua kama asafirishwe au azikwe huku
 
“Mama yake alikuwa amekwenda Lubumbashi, lakini sasa inabidi ageuze na ndege, akisharudi ndiyo tutajua kama tunazika au tunasafirisha…… mama yake ni dada yangu, kwahiyo Ndanda ananiita mimi mjomba”



Hadi mauti yanamkuta Ndada alikuwa akifanya shughuli za muziki kama msanii wa kujitegemea ‘Solo Artist’ pamoja na shughuli za kibiashara

Tuesday, April 5, 2016

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono afariki usingizini

Image captionAliyekuwa nyota wa filamu za ngono Meghan Wren
Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Amber Rayne amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles ,maafisa wamethibitisha.
Marafiki na waliokuwa wafanyikazi wenzake walituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wakimuenzi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alifariki usingizi wikendi iliopita.
Amber alikuwa nyota wa filamu za ngono kwa muongo mmoja kabla ya kujiuzulu mwaka 2015.
Alikuwa miongoni ,mwa kundi moja la wanawake ambao walidai kwamba James Deen,ambaye pia ni nyota wa filamu za ngono alimshambulia.
Hatahivyo Deen amekana madai hayo.
Mkaguzi wa matibabu katika kaunti ya Los Angeles ameiambia Newsbeat kwamba hakuna sababu rasmi ya kifo chake iliothibitishwa.
Hatahivyo wamesema kuwa familia yake imearifiwa.Bi Rayne ,ambaye jina lake rasmi ni Meghan Wren,alitangaza kujiuzlu kutoka kazi hiyo mwaka uliopita.
Wafanyikazi wenza katika soko la filamu za ngono walituma ujumbe wa kushtushwa na kifo chake.

Saturday, April 2, 2016

Burundi: Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara afariki ghafla


Kifo cha waziri wa zamani wa Rwanda katika gereza la Mpimba mjini Bujumbura, chazua maswali mengi, Machi 30, 2016.
Kifo cha waziri wa zamani wa Rwanda katika gereza la Mpimba mjini Bujumbura, chazua maswali mengi, Machi 30, 2016.
© REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimama


Waziri wa zamani na mwanadiplomasia wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara, ambaye alikuwa balozi nchini Ufaransa na Ubelgiji, amefariki ghafla Jumatano hii Machi 30 katika gereza kuu la Mpimba mjini Bujumbura , ambako alikuwa akizuiliwa tangu Desemba 2015.

Mwanadiplomasia huyo wa zamani wa Rwanda alikua akituhumiwa na utawala wa Nkurunziza kuwa aliingia Burundi kufanya ujasusi.
Vyanzo vya ndani vya gereza kuu la Mpimba vinaeleza wazi: Jacques Bihozagara alikua na hali"nzuri" jana asubuhi. Lakini baadae mchana alihisi hali yake haiko sawa, akachukua uamuzi wa kwenda hospitali ilio ndani ya gereza. Wafungwa wenzake wanahakikisha kuwa"walishangaa" kusikia baada ya dakika ishirini kuwa Waziri huyo wa zamani wa Rwanda amefariki.
Nini kilichotokea katika hospitali hii? Ni sababu ipi ya kifo chake? maswali yote haya yamekosa majibu, wakati ambapo mkurugenzi wa gereza la Mpimba amekataa kujieleza juu ya kifo hicho Jumatano hii Alaasiri.
Balozi wa Rwanda nchini Burundi, Amandin Rugira, amethibitisha taarifa kwenye Twitter, akitangaza kwamba bado hajajua sababu za kifo chake. Afisa mwandamizi kwenye wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda ambaye amewasiliana na RFI amesema wazi. Amehakikisha kwamba Rwanda "ilishtushwa" na taarifa hiyo, huku akibaini kwamba serikali ya Rwanda inaamini kwamba mwanadiplomasia huyo mstaafu alikuwa kizuizini kinyume cha sheria. Na ameongeza : "Tunaomba mamlaka ya Burundi kutoa mwanga juu ya kifo cha ghafla ambacho kiinaibua maswali mengi. "
Bw Bihozagara, alikua akijihusisha na biashara tangu alipostaafu, alikuwa amewekeza nchini Burundi, nchi ambapo alizaliwa na aliishii katika ujana wake, na alikua akiingia nchini humo mara kwa mara kwa ajili ya biashara yake. Alikamatwa Desemba 4, 2015 na Idara ya Ujasusi ya Burundi, ambayo inasimamiwa moja kwa moja na Rais Pierre Nkurunziza. Idara hiyo imekua ikimshtumu "kufanya ujasusi kwa maslahi ya nchi yake" wakati ambapo kunashuhudiwa mdororo wa mahusiano kati ya nchi hizo mbili, kwa sababu ya mgogoro wa kina unaoikabili Burundi kwa sasa.
Kifo cha afisa wa zamani muhimu katika serikali ya Rwanda katika gereza la Burundi kinaweza kukuza uadui zaidi katika mahusiano ambayo tayari yamekwisha ingiliwa na dosari. Tayari katika mitandao ya kijamii, watu wengi wanahitaji kuona msimamo mkali wa Rwanda wakati upande mwengine, wamekua kimya na aibu ikitawala.