Ulimwengu wa muziki
unaomboleza kifo cha mwanzilishi wa vyombo vya muziki vya Roland
Ikutaro Kakehashi, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 87.
Mhandisi huyo raia wa Japan aligundua vyombo vingi vya kupiga ngoma kikiwemo chombo cha TR-808Vyombo hivyo vimetumiwa kwa muziki wa hip-hop na kutumiwa na wanamuziki wrngi wakiwemo Kanye West hadi Marvin Gaye.
Kakehashi alipewa tuzo la kiufundi la Garmmy mwaka 2013 kwa mchango wake katika teknolojia ya muziki.
Kabla ya kuongoza Roland kwa miaka 40, bwana Kakehashi alianzisha kampuni ya Ace Tone miaka ya sitini..
Sauti ya chombo cha muziki cha TR-808 ilileta mabadiliko makubwa kwenye muziki miaka themanini na tisini.
Albamu yake Kanye West ya mwaka 2008 ya 808s & Heartbreak, inakionyesha chombo hicho wakati wote.
Haki miliki ya picha Facebook / Tommy Snyder
No comments:
Post a Comment