Showing posts with label MICHEZO KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO KIMATAIFA. Show all posts

Sunday, April 2, 2017

SAMATTA ATUPIA KRC GENK IKIIBANJUA LOKEREN 4-0

3
Kipenzi cha  wa Tanzania na Nahodha wa Stars Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao moja timu yake, KRC Genk ikishinda 4-0 Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk dhidi ya Lokeren katika mchezo wa mchujo wa kuwania kucheza UEFA Europa League msimu ujao Mchezo wa kundi B.
Samatta alifunga bao lake dakika ya 72, likiwa la pili katika mchezo huo baada ya Alejandro Pozuelo kutangulia kuifungia Genk la kwanza dakika ya 45 na  kabla ya Jean-Paul Boetius kufunga la tatu dakika ya 77 na Jose Naranjo kumalizia la nne dakika ya 90.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen, Berge, Pozuelo, Malinovskyi/Heynen dk68, Trossard, Boetius/Buffalo dk83 na Samatta/Naranjo dk79.
Lokeren: Verhulst, Maric, Skulason, Person, De Sutter, Galitsios, Ofkir, Hupperts/Stra Sunsetman dk61, Ticinovic/De Prycker dk77, na De Ridder Bolbat/Martin dk58.

Wednesday, June 8, 2016

Bomu laua watu kadhaa Istanbul

Watu 11 wameuawa na wengine wapatao 36 wamejeruhiwa baada ya bomu la kutegwa kwenye gari kulipuka Istanbul, Uturuki. Bomu liliwalenga polisi na lililipuka wakati watu wengi walikuwa wakielekea kazini.
Magari ya kusafirisha wagonjwa yaliendeshwa kwa kasi katika mitaa ya Istanbul kuchukua waliojeruhiwa katika mlipuko wa bomu. Bomu hilo lililokuwa limetegwa kwenye gari lililipuka pale ambapo mabasi ya polisi yalipopita karibu nalo. Mlipuko uliharibu pia majengo na magari mengine yaliyokuwa karibu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu, amelaani shambulio hilo akisema washambuliaji wana roho ngumu kulipua mabomu wakati wa Ramadhani.
Akitoa maelezo zaidi kuhusu mlipuko, Gavana wa Istanbul, Vasip Sahin amesema: "Bomu la kutegwa garini lililipua magari yaliyokuwa yakibeba polisi wetu wa kikosi maalumu na yalipokuwa yakipita barabarani saa mbili na dakika arobaini asubuhi. Bomu limesababisha vifo vya polisi saba na raia wa kawaida wanne. Mungu azirehemu roho zao. Watu 36 wamejeruhiwa. Upelelezi unaendelea."
Historia ndefu ya vita na PKK
Gari la polisi lililoshambuliwa na bomu Istanbul Gari la polisi lililoshambuliwa na bomu Istanbul
Istanbul ndio jiji kubwa zaidi nchini Uturuki na hii ni mara ya nne kwa jiji hilo kushuhudia shambulio kubwa la bomu ndani ya mwaka huu. Bado hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio la Jumanne lakini wanamgambo wa chama cha Kikurdi cha PKK kilichopigwa marufuku, wamekuwa wakifanya mashambulio kama hayo katika siku za nyuma, likiwemo shambulio moja hapo hapo Istanbul mwezi uliopita.
Chama cha PKK ambacho kiko kwenye mgogoro na serikali ya Uturuki tangu mwaka 1984, mara kwa mara wapiganaji wake wamekuwa wakishambulia magari ya polisi na ya jeshi kwa kulipua mabomu ya kwenye magari.
Pamoja na hayo, wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu wamelaumiwa kwa kulipua mabomu kadhaa Uturuki. Inakadiriwa kwamba maafisa wa usalama wapatao 500 wa Uturuki wameuliwa katika mashambulio kama hayo au katika mapambano na wanamgambo wa Kikurdi. Kwa upande mwingine, jeshi la Uturuki linadai kuwa limefanikiwa kuwaua wapiganaji wa PKK wapatao 5,000 katika operesheni zinazoendeshwa Uturuki kwenyewe na Iraq ya Kaskazini ambapo PKK ina ngome kubwa.
PKK inataka Wakurdi wanaoishi Kusini Mashariki mwa Uturuki waweze kujitawala wenyewe. Mapigano kati ya majeshi ya serikali na chama hicho yamekuwa yakiendelea kwa miongo kadhaa na mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu wapatao 40,000.

Tuesday, May 31, 2016

Nick Cannon kaweka dola laki moja mezani kwa anayeweza kushindana naye kuchana.

Rapa,Mwigizaji na mtangazaji Nick Cannon ameweka dola laki moja mezani kwa rapa yoyote nchini Marekani anayeweza kushindana naye kuchana wafanye RAP BATTLE.
Kupitia twitter Nick Cannon amesema ana dola $100,000 kwa rapa atakaye mshinda ataipata, ila pia huyu rapa aweke chini dola laki moja,akishindwa anaipoteza.
Shindano litafanyika kwenye tuzo za 2016 BET Awards  mjini Los Angeles  mnamo  June 25.
Battle rap iliwahi kufanyika kwenye tuzo za BET kati ya Snoop Dogg na Murda Mook kupitia “Gladiator School” na ilikuwa BET Hip Hop Awards  mjini Atlanta mwaka 2014

CONFIRMED: Cristiano Ronaldo hatocheza mchezo dhidi ya England June 2 2016

Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos  leo Jumatatu ya May 30 2016, amenukuliwa na vyombo vya habari hususani dailymail akithibitisha kuwa katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake dhidi ya timu ya Uingereza utakaochezwa June 2 2016 katika uwanja wa Wembley Cristiano Ronaldo na Pepe hawatocheza.
Fernando Santos amesema hayo kutokana na nyota hao kuwa na uchovu, kwani toka wamalize mchezo wa fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu yao ya Real Madriddhidi ya Atletico Madrid uliochezwa May 28 2016 Milan Italia, hawajapata muda wa kupumzika hivyo wanahitaji wiki moja ya kupumzika.
pepe_cristiano
Ronaldo na Pepe
“Siwapumzishi kwa sababu ya kukwepa majeruhi ila ni kwa ajili ya kuwaweka fiti tu, nafikiri Cristiano Ronaldo atajiunga na timu Jumamosi akiwa na hali ya kujiamini, ni mchezaji bora wa dunia na yeye ni muhimu kwa timu”

Man United wamefanya maamuzi mapya kuhusu hatma ya Marcus Rashford

Klabu ya Manchester United ya Uingereza leo May 30 2016 imetangaza maamuzi mapya ambayo yatawapa furaha mashabiki wa klabu hiyo, Man United leo May 30 imetangaza kumpa mkataba wa miaka minne kinda aliyekuja kwa kasi Marcus Rashford.
Man United wamempa mkataba huo wa miaka minne utakamuoweka staa huyo Old Trafford hadi June 2020, Rashford mara ya kwanza kucheza mechi na kikosi cha kwanza cha Man United alifunga magoli mawili katika mchezo dhidi ya Midtjyllandmwezi February.
UnitedÂ’s Marcus Rashford celebrates after scoring  during the Europa League round of 32 second leg soccer match between Manchester United and FC Midtjylland in Manchester, England, Thursday, Feb. 25, 2016 . (AP Photo/Jon Super)
Kutoka kushoto ni Marcus Rashford na Cameron Borthwick-Jackson waliposaini mikataba yao
Kinda huyo wa Man United amefanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 akiifungia Man United jumla ya magoli 8 katika mechi 18 alizoichezea klabu hiyo msimu huu, Rashfordkwa sasa ana umri wa miaka 18 na alianza kuichezea timu ya vijana ya Man United toka mwaka 2005, kinda huyo pia ameitwa katika kikosi cha England cha wachezaji 26 watakaoshiriki michuano ya Euro 2016.

UEFA wametangaza majina 18 ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha mwaka 2016, England hakuna hata mmoja

Ni siku mbili zimepita toka tushuhudia ile fainali ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya kwa mwaka 2016, fainali ambayo ilichezwa katika uwanja wa San Siro Milan Italia, hiyo ilikuwa fainali inayozihusisha timu kutoka nchi na jiji moja Hispania Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid.
Leo May 30 2016 shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 18 kutoka timu mbalimbali barani Ulaya na kuwataja kama ndio wachezaji waliofanikiwa kuunda kikosi bora cha msimu wa 2015/2016 kwa UEFA, list ya wachezaji hao waliotajwa hakuna hata jina la mchezaji yoyote kutoka Ligi Kuu Uingereza.
Ni vilabu vitano tu ndio vimefanikiwa wachezaji wake kutajwa katika list ya wachezaji 18 wa UEFA kwa msimu wa 2015/2016, Atletico Madrid na Real Madrid zimetoa wachezaji sita sita, wakati FC Barcelona imetoa wachezaji watatu, FC Bayern Munich imetoa wachezaji wawili na Paris Saint Germain imetoa mchezaji mmoja.
longUCLenglish
ALL GOALS: Fainali ya FA CUP May 

Friday, May 27, 2016

PICHA: Jose Mourinho amesaini Man United, taarifa rasmi kutoka Sky Sport

Huenda huu ndio ukawa mwisho wa headlines za Jose Mourinho kuhusishwa kujiunga na klabu ya Man United, kwani taarifa kutoka mitandao mingi ya soka Ulaya ikiwemo Sky Sport unaripoti kocha huyo kujiunga na Man United.
Sky Sport wameripoti Jose Mourinho kusaini mkataba rasmi na Man United, kinachosubiriwa ni uongozi wa klabu hiyo kumtangaza tu, kwani leo May 26 ameonekana katika hoteli London akiripotiwa kuwa alikuwa na kikao na mtendaji mkuu wa Man United Ed Woodward.
Video ya ripota wa Sky Sport akithibitisha Jose Mourinho kujiunga Man United bonyezahapa
sav
ALL GOALS: Fainali ya FA CUP May 25 2016 Yanga vs Az

Monday, May 23, 2016

Man United kumtangaza Jose Mourinho kama kocha wao

Usiku wa May 21 2016 vyombo vingi vya habari za michezo barani Ulaya vinategemea kuandika stori tofauti na iliyozoeleka kuhusu tetesi za Jose Mourinho, tetesi zilizopo kwenye headlines kwa muda mrefu ni kuhusu klabu ya Man United kuripotiwa kuwa itampa Jose Mourinho kazi ya kuifundisha klabu yao.
Hiyo ndio habari iliyopo kwenye headlines kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa, lakini leo May 21 2016 ndio imeripotiwa na Metro na gazeti la Hispania AS kuwa baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la FA utakaochezwa leo katika uwanja wa Wembley, kati ya Man United dhidi ya Crystal Palace, Man United watamtangaza Mourinho kuwa kocha wao.
Matokeo ya mchezo wa fainali leo May 21 2016 hauwezi kuokoa kibarua cha kocha Louis van Gaal hata kama  atafanikiwa kutwaa taji hilo, kwani uongozi wa Man United haujafurahishwa na Man United kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Manchester United yamfuta kazi Louis van Gaal


Image caption Louis Van Gaal
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

Monday, May 16, 2016

AZAM FC ‘WANASHANGAZA’ SANA KATIKA MACHAGUO YAO YA MAKOCHA

IMG-20160513-WA0012
IMG-20160513-WA0012
AZAM FC wanashangaza sana kwa kweli! Ukiniuliza Azam inahitaji nini zaidi? Jibu langu ni kocha bora mwenye uzoefu na mpira wa Afrika. Mfano, Mnigeria, Stephen Keshi ama pengine Mscotland, Bobby Williamson ambaye kwa miaka nane amekuwa na kazi yenye mafanikio katika Afrika Mashariki na Kati.
Sijui lolote kuhusu kocha Mspaniola ambaye ameingia nchini Ijumaa kufanya mazungumzo ya kukinoa kikosi hicho ambacho kwa hakika kitashiriki katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika baadae mwaka ujao.
Nilikwisha andika mara kadhaa kuhusu uwezo wa kiufundishaji wa kocha wa sasa Muingereza, Stewart Hall ambaye kwa mara ya tatu ndani ya miaka minne ataachia kazi. Azam FC imejipotezea muda kwa uamuzi wake wa kumrejesha Hall ili kuchukua nafasi ya Mhindi, Boris Bunjak mara baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2012/13.
Hall alijiunga kwa mara ya kwanza na Azam FC mwezi Disemba  2010 akitokea Zanzibar alikokuwa akiinoa timu ya Taifa ‘Zanzibar Heroes.’
Kabla yake Azam ilikuwa ilifundishwa na Wabrazil, Neider Santos ambaye alikuwa kocha wa kwanza kuifundisha timu katika Ligi kuu msimu wa 2008/09, kisha akafuata aliyekuwa msaidizi wa Santos, raia mwenzake wa Brazil, Itamor Amourin ambaye alikinusuru kikosi hicho kutoshuka katika msimu wao wa kwanza VPL.
Itamour alikuja kuondolewa kwa kuwa Azam ilihitaji kocha atayewapa mafanikio ya haraka katika VPL ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya CAF. Hall aliamalizia msimu wa 2010/11 na kuisaidia Azam kumaliza nafasi ya tatu katika ligi kuu.
Nafasi hiyo iliwapa tiketi ya kucheza michuano ya CECAFA Kagame Cup kwa mara ya kwanza mwaka 2012. Msimu wa 2011/12 Muingereza huyo akaisaidi Azam kumaliza katika nafasi ya pili katika VPL, kisha kuifanikiwa kufika fainali katika michuano yao ya kwanza za kimataifa (Kagame Cup 2012) mchezo ambao walipoteza 2-0 dhidi ya Yanga SC.
Hall akafukuzwa kazi kwa kile kilichodaiwa kukaidi maagizo ya bosi wake kutomchezesha kiungo mshambulizi, Mrisho Ngassa katika mchezo wa fainali. Ngassa aliibusu na kuvaa jezi ya Yanga wakati alipofunga goli pekee la Azam akitokea benchi katika pambano la nusu fainali dhidi AS Vita Club ya DR Congo.
Hall aliondolewa kwa sababu zisizo za kimpira na mtu aliyechukua nafasi yake Agosti 2012, Bunjak hakufaa kwa maana tayari Azam ilikuwa imesogea mbele kiuchezaji. Makosa ya kumtimua Hall yaliigarimu sana timu hiyo kwa kuwa wachezaji wa Azam wanampenda sana kocha huyo. Akarudishwa miezi mitatu baadae na kuisaidia tena Azam kumaliza katika nafasi ya pili ya ligi kuu msimu wa 2012/13.
Katika michuano ya Shirikisho Afrika mwaka 2013 ambayo ilikuwa ni ya kwanza kwa Azam FC katika michuano ya CAF, Hall alifanikiwa kuisaidia Azam kufika hadi hatua ya 16 bora. Alikuwa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa na Azam ilionekana inahitaji zaidi taji la ligi kuu.
Miaka mitatu iliyopita wakati Azam ilipozidiwa dakika za mwisho na Yanga katika michezo ya VPL na kushindwa kutwaa ubingwa msimu wa 2012/13 nilishauri kuwa timu hiyo inapaswa kusaka kocha mwenye mbinu zaidi ya Hall ili wapate ubingwa wao wa kwanza wa VPL.
Hall licha ya vikosi vyake kucheza vizuri, mbinu zake katika michezo ya kuamua ubingwa hazijawahi kuwa bora. Hata msimu huu amefanikiwa kupata pointi nne tu katika michezo minne dhidi ya washindani wake wakubwa katika taji, timu za Yanga na Simba.
Hata wakati ule alipoisaidia kumaliza katika nafasi ya pili msimu wa 2011/12 na 2012/13 Hall alishindwa katika mipambano muhimu dhidi ya washindani wake wa ubingwa. Aliondolewa mara baada ya kumalizika kwa michezo ya mzunguko wa kwanza VPL msimu wa 2013/14 na nafasi yake ikaangukia kwa Mcameroon, Joseph Omog ambaye alikuwa mshindi wa kombe la Shirikisho Afrika mwaka mmoja nyuma akiwa na timu ya AFC Leopard ya Congo Brazzaville.
Omog aliipa Azam FC ubingwa wa kwanza wa VPL Mei 2014 huku mbinu zake dhidi ya Yanga na Simba zikiwa ni kusaka matokeo zaidi. Alifukuzwa baada ya Azam kupoteza 3-0 ugenini dhidi ya El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika, Februari 2015.
Hall akarejeshwa mara baada ya kumalizika kwa msimu wa 2014/15. Ameisaidia Azam FC kushinda ubingwa wa kwanza wa Kagame Cup Julai 2015 lakini katika ligi ameendelea kuchemsha. Amekuwa mlalamishi mno kuhusu waamuzi hasa timu yake inaposhindwa kupata matokeo.
Kama unakumbuka baada ya Azam kuchapwa 3-0 na Esperance ya Tunisia na kuondolewa kwa jumla ya magoli 4-2 katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Shirikisho niliandika kuwa Azam inahitaji kocha mpya mwenye mbinu, uzoefu na mpira wa Afrika na nikatolea mfano mshindi wa CAN 2013, Keshi.
Ila wamemleta mtu mpya kabisa na Afrika, kigezo kikubwa ni nchi anayotoka. Naye tutamfahamu kisha tutajua kama ni chaguo sahihi au ataiporomosha timu hiyo kutoka ilipo sasa ‘TOP 2 VPL’ kwa misimu mi 4 mfululizo.

Shabiki wa Man Utd usisome hii – Di Maria aweka rekodi hii ya utoaji wa assist Ufaransa

Takribani mwaka mmoja baada ya kuwa uhamisho ghali uliofeli katika klabu ya Manchester United – Angel Di Maria ameonyesha kwanini Louis van Gaal alikosea kumuuza kwenda PSG.
image
Kiungo mshambuliaji wa PSG ametengeneza rekodi mpya kwenye ligi ya Ligue 1 kuwa kutoa pasi 18 zilizosababisha magoli kwenye msimu huu.  
Di Maria aliwatengenezea magoli Zlatan Ibrahimovic na Lucas Moura katika mchezo wa ushindi wa 4-0 wa PSG dhidi ya Nantes.
Rekodi ya nyuma iliyokuwepo ilikuwa assists 17 ambayo iliwekwa na Marvin Martin wakati akiichezea FC Sochaux msimu wa 2010-11.
Di Maria aliuzwa na Manchester United baada ya kuitumikia kwa msimu mmoja – PSG walilipa kiasi cha £44 million mnamo mwezi August 2015 ili kupata huduma za kiungo huyo wa Argentina.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 tayari ameshashinda ubingwa wa Ligue 1 na pia anaweza kushinda kombe la Ufaransa ikiwa PSG wataifunga Marseille katika mchezo wa fainali baadae mwezi huu.

PICHA & VIDEO: Kikosi cha uteguaji mabomu kilivyowasili Old Trafford kufanya uchunguzi wa bomu

May 15 2016 michezo ya mwisho ya kukamilisha Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016 iliendelea kama kawaida, ila mchezo kati ya Man United dhidi ya AFC Bournemouth uliyokuwa uchezwe katika uwanja wa Old Trafford umeahirishwa kutokana uwanja huo kuhofiwa kutokuwa na hali nzuri ya kiusalama.
3432E53800000578-3591435-Police_and_sniffer_dogs_were_in_the_ground_after_they_were_told_-a-48_1463323680639
Mchezo huo umehairishwa muda mchache ukiwa unatazamiwa kuanza, hiyo kutokana na uwanja wa Man United Old Trafford ambao una uwezo wa kuchukua mashabiki 75000 kuhisiwa kuwa bomu, hivyo kutokana na hali za kiusalama, mashabiki waliokuwa wameingia uwanjani kuangalia mchezo huo kuanza kutolewa nje.
3432FCE000000578-3591435-A_bag_is_searched_in_the_stands_prior_to_the_match_being_abandon-a-59_1463323680912
Baada ya kuahirishwa kwa mchezo huo kati ya Man United dhidi ya AFC Bournemouth, ratiba ya lini utachezwa mchezo huo imetajwa kuwa ni Jumanne ya May 17 2016.
3432FB7000000578-3591435-At_around_3_20pm_the_remaining_fans_from_all_the_stands_began_to-a-57_1463323680860
34341E4200000578-3591435-image-a-21_1463335648741 (1)
Rashford alipokuwa akiondoka Old Traford baada ya kuambiwa sehemu hiyo sio salama,
VIDEO WACHAMBUZI WA SOKA WALIVYOKUWA NJE WAKATI WA KIKOSI CHA UTEGUAJI MABOSI KIKIWASILI OLD TRAFFORD

VIDEO: Top 10 ya mashambulizi hatari yaliompita kipa, yakaokolewa na beki

May 15 2016 mtu wangu wa nguvu ambaye unapenda mchezo wa mpira wa miguu, naomba nikukutanisha na mashambulizi hatari ndani ya mchezo wa soka yaliofanikiwa kuokolewa dakika za mwisho na mabeki baada ya golikipa kupitwa, haya ni mashambulizi ambayo mabeki wameokoa katika position ambazo asilimia kubwa inaaminika kuwa mpira utaingia wavuni.

Sunday, May 8, 2016

VIDEO: Siku moja baada ya kumpoteza Patrick Ekeng uwanjani, haya ni matukio 9 ya kusikitisha katika soka

Bado dunia ya soka inakumbuka na kuomboleza kifo cha staa wa soka wa Cameroonaliyekuwa anakipiga katika klabu ya Dinamo ya Romania Patrick Ekeng ambaye alianguka uwanjani May 6 2016 na kupoteza maisha dakika ya 70. Haya ni baadhi ya matukio 9 ya kusikitisha katika soka

Saturday, May 7, 2016

VIDEO: TOP 20 ya Ball Control Skills za Lionel Messi, Ronaldo, Neymar na mastaa wengine



Najua mtu wangu wangu huwa unapenda soka na kila weekend hupendi upitwe na mechi kali, hususani zinazohusisha mastaa wako unaowakubali kama NeymarLionel Messi naCristiano Ronaldo, huenda hii hukuwahi kukutana nayo, naomba nikusogezee dakika 3 na sekunde 49 za ujuzi na njonjo za mastaa wako katika kuuchezea mpira
.

Tuesday, May 3, 2016

Hii ndio klabu ya kwanza kupanda Ligi Kuu Uingereza msimu ujao 2016/2017

Wakati Ligi Kuu Uingereza ikiendelea kwa vilabu vya Tottenham Hotspurs na Leicester City kuchuana kwa karibu katika mbio za kuwania Ligi Kuu Uingereza, huku vilabu vya Newcastle UnitedSunderlandNorwich City vikiwa katika hatua ya kupigania kutoshuka daraja na Aston Villa kuonesha dalili zote za kushuka, Bunley imekuwa klabu ya kwanza kurudi Ligi Kuu Uingereza msimu ujao.
nbm
Bunley wamefanikiwa kupanda Ligi Kuu Uingereza na watashiriki Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2016/2017, nafasi hiyo wameipata baada ya kushinda kwa goli 1-0 dhidi yaQPRBunley wanarejea Ligi Kuu Uingereza wakiwa hawajafungwa mchezo wowote toka siku ya Boxing Day.

Monday, May 2, 2016

Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL



Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 2 Mei, 2016.
NambariKlabuMechiMabaoAlama
1Leicester363077
2Tottenham353969
3Arsenal362567
4Man City363064
5Man Utd351260
6West Ham351759
7Southampton361457
8Liverpool351155
9Stoke36-1448
10Chelsea34747
11Everton35644
12Watford35-644
13Swansea36-1343
14West Brom36-1441
15Bournemouth36-2041
16Crystal Palace36-1039
17Newcastle36-2533
18Sunderland35-1832
19Norwich35-2631
20Aston Villa36-4516

Leicester City kunyemelea ushindi Epl?

Image copyrightbbc
Image captionLeicester City imetoka sare ya 1-1 ilipokutana na Manchester United
Leicester City wamebakiwa na alama mbili pekee kuupata ushindi wa ligi kuu ya England baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya klabu ya Manchester United katika dimba la Old Trafford huku wakitegemea matokeo ya mchezo kati ya Chelsea dhidi ya Tottenham utakaopigwa leo hii majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki katika dimba la Stamford Bridge.
Mbweha walipata afueni baada ya kuwa nyuma kwa goli moja lililofungwa na Antony Martial dakika ya nane ya mchezo kabla ya kusawazisha na kepten Wes Morgan dakika ya 17. Pande zote mbili zilinyimwa mikwaju ya penalti baada ya mlinzi Marcos Rojo kumzuia Riyad Mahrez ndani ya eneo la 18 huku pia Danny Drinkwater wa Leicester akimvuta Memphis Depay ndani ya eneo la hatari.
kwa matokeo hayo Leicester wanaendelea kubaki kileleni mwa ligi ya England wakiwa na alama 77. Claudio Ranieri huyo akisisitiza kuwa hawakufuata kikombe OT bali kucheza mchezo safi lakini Man U walikua wazuri zaidi yao. Matokeo mengine Liverpool walikiona cha mtema kuni baada ya kuchapwa 3-1 walipokuwa wageni wa Swansea huku Man city wakiambulia kichapo cha mbwa mwizi 4-2 walipowatembelea Sauthampton