Adam Johnson akitoka mahakamani
LEO Machi 24, za kusikitisha katika ulimwengu wa soka zimezidi kutawala, ikiwa umepita muda mchache tu toka utangazwe msiba wa nguli wa soka wa Uholanzi na FC Barcelona Johan Cruff, ila zimetoka taarifa za staa wa soka kufungwa jela.
Winga wa zamani wa klabu ya Manchester City na timu ya Taifa ya Uingereza, Adam Johnson amehukumiwa miaka sita kwenda jela baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15.
Adam Johnson hadi anahukumiwa kifungo hicho alikuwa anaitumikia klabu ya Sunderland ya Uingereza, ambayo toka mwaka 2012 alijiunga nayo hadi 2016, ameichezea jumla ya mechi 122 na kuifungia magoli 19
No comments:
Post a Comment