Marekani na washirika wake kutoka Ulaya wameulalamikia Umoja wa Mataifa kuhusu hatua ya Iran ya kufanyia majaribio makombora ya masafa marefu.
Mataifa hayo yamesema majaribio hayo yanakiuka azimio la Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo ambalo liliidhinisha mkataba wa nyuklia baina ya UN na Iran liliitaka Iran kutofanyia majaribio makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.
Kwenye barua, iliyopatikana na Reuters, maafisa wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani wameeleza wasiwasi wao kuhusiana na madai ya Iran kwamba makombora hayo yameungwa mahususi kuwa tishio kwa Israel.
Mataifa hayo manne yameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili hatua zinazofaa kuchukuliwa.
Hata hivyo, hayakusema waziwazi kwamba majaribio hayo ya makombora yanakiuka azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Iran.
Makombora hayo yalikuwa yameandikwa kauli mbiu: “Israel sharti iangamizwe”, ikiwa imeandikwa kwa Kiyahudi.
No comments:
Post a Comment