China kuisadia Kenya kuwa kituo cha mafunzo ya mambo ya reli
Katibu Mkuu wa wizara ya usafirishaji na miundombinu wa Kenya Bw Irungu Nyakera, amesema China itaisaidia Kenya kuwa kituo cha mambo ya reli kwenye eneo la Afrika Mashariki na kati.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Nairobi Bw Nyakera amesema kampuni ya ujenzi wa barabara na madaraja ya China, itatoa dola milioni 10 kwa ajili ya kuinua kiwango cha taasisi ya mafunzo ya mambo ya reli ya Kenya.
Mbali na fedha hizo, China pia inatoa mafunzo kwa wahadhiri 10 wa taasisi ya mafunzo ya reli, na wengine 40 wanatarajiwa kuja China kwa ajili ya mafunzo kama hayo katika miezi ijayo. China na Kenya pia zinafanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya vyuo vikuu vya pande mbili kwenye eneo la uhandisi.

No comments:
Post a Comment