Tuesday, March 29, 2016

Marais wa China na Czech wakutana mjini Prage



Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Czech Milos Zeman mjini Prague na kubadilishana naye maoni kuhusu masuala ya uhusiano kati ya nchi zao na kati ya China na Ulaya..
Rais Xi amesema katika miaka ya hivi karibuni, China na Czech zimepata maendeleo makubwa katika uhusiano na ushirikiano wao, na mwaka jana zilisaini makubaliano ya kiserikali ya kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kuweka msingi mzuri wa uhusiano kati yao. Pia amesema China imekuwa inaunga mkono utandawazi wa Ulaya na kufurahia kuona Umoja wa Ulaya wenye ustawi, umoja na utulivu, na inapenda kutoa mchango katika kuimarisha ushirikiano na nchi za Ulaya.
Kwa upande wake rais Zeman amesema, Czech inazingatia uhusiano kati yake na China, na ana imani kuwa, ziara ya rais Xi itaongeza uaminifu wa kisiasa kati ya pande mbili, na kuziletea nchi hizo mbili fursa mpya za ushirikiano. Pia amesema Czech inapenda kuwa mshirika wa China katika Umoja wa Ulaya.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment