Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar kwa kutokuwa wa wazi na haki pamoja na kushindwa kutekeleza Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea ufadhili wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.
Taarifa ya Bodi imesema: “Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”
Aidha imeongeza kuwa Tanzania iliamua kuendelea na uchaguzi bila kuzingatia kuwa Upande wa Wapinzani wao CUF na kushindwa kuakisi malalamiko kutoka Serikali ya Marekani na jamii ya Kimataifa.”
Mabalozi wakosoa Uchaguzi wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment