Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry pamoja na Balozi wa masuala ya wanawake Cathy Russell wakipiga picha na washindi wa tunzo ya "Wanawake Shujaa" 2016.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, aliwakabidhi wanawake kumi na wanne kutoka nchi mbali mbali za dunia tuzo ya Wanawake Shujaa, kwa kuonyesha uongozi katika kutetea haki, haki za binadam, demokrasia, usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake.
Mmoja kati ya walopokea tuzo hiyo maarufu inayotolewa kila mwaka na Marekani, ni mwanaharakati wa kichina, Ni Yulan, aliyezuiliwa na serikali yake kusafiri hadi Washington.
Miongoni mwa wanawake watatu kutoka Afrika ni Vicky Ntetema, Mtanzania aliyetunukiwa tuzo hiyo kwa jitihada zake za kufichua mbinu zinazotumika kuwauwa na kuwakata viungo watu wenye ulemavu wa ngozi – albino.
Waziri Kerry amesema, “Mwaka huu tunatambua kundi la wanawake walonesha ushujaa katika fani tatu muhimu. Kufichua na kupinga ghasia kwa misingi ya ngono, wanapambana na ulaji rushwa na kuimarisha utawala wa sheria na wanaohamasisha haki za kisheria na haki za binadamu kwa wote.”
Huu ni mwaka wa 10 tangu kuanzishwa kwa tunzo ya “Women of Courage”, ambapo hasi sasa wanawake 101 wamepokea tunzo hiyo kutokana na mafanikio yao.
No comments:
Post a Comment