Seif a-Din Mustafa aliilazimu ndege hiyo iliyokuwa inakwenda Cairo kugeuza njia kwa kujifanya amevaa ukanda wa vilipuzi kiunoni mwake.
Anasemakana kukabiliwa na matatizo ya akili.
Polisi wa Cyprus wanasema Seif a-Din Mustafa - ambaye ana zaidi ya miaka 50 anakabiliwa na mashtaa kadhaa atakapowasili kotini leo.
Jamaa zake huko Cairo, wamehojiwa kama sehemu ya uchunguzi unaoendelea dhidi ya hatua yake ya kuiteka ndege ya EgyptAir MS 181.
Tukio hili lisilo la kawaida lililosababisha mkwamo wa saa sita katika uwanja wa ndege wa Larnaca linadhaniwa kuwa limechchewa kwa mzozo kati ya mtekaji huyo na aliyekuwa mkewe - anayeishi Cyprus.
Zaidi ya watu 60 waliokuwa kwenye ndege hiyo - wakiwemo Waingereza wanne - hatimaye waliachiliwa huru pasi kujeruhiwa. Wahudumu wa ndege hiyo sasa wamerudi Cairo - ambako walijumuika na familia zao kwa furaha kuu katika uwanja wa ndege.
No comments:
Post a Comment