Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amesikitishwa na kikosi chake kukosa ubunifu baada ya kufungwa 2-1 Uholanzi.
Kipigo hicho kimekuja baada ya Uingereza kuonyesha kiwango bora wakitoka nyuma na kuwafunga mabingwa wa dunia Ujerumani mabao 3-2.
Akizungumza baada ya mchezo huo Hodgson amesema pamoja na kumiliki vyema mpira lakini wachezaji wake hawakuwa wabunifu jambo lilichangia kutotengeneza nafasi za kutosha.
Meneja huyo aliongeza kuwa hawakucheza vyema kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Ujerumani kule Berlin.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Uingereza katika Uwanja wa Wembley tangu Novemba mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment