Ebola sio janga tena la kiafya na hatari ya kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo ni kidogo, Shirika la afya duniani WHO linasema.
Visa kidogo bado vinatokea Guinea, lakini Sierra Leone na Liberia bado hazijashuhudia visa vyo vyote kwa miezi kadhaa.
Lakini wataalamu wanasema ni lazima nchi ziwe waangalifu kwa ongezeko la visa vipya.
Vimetokea mara 12 mpaka sasa - vya hivi karibuni ni Machi 17 nchini Guinea.
WHO linasema nchi zimeweza kuwajibikia haraka visa hivi kuvidhibiti.
Na msururu wa maambukizi ya Ebola umeisha katika nchi tatu za Afrika magharibi ambazo ziligubikwa kwa janga hilo.
Ebola husambaa kwa kumgusa mtu. Virusi hupatikana kwenye maji ya mwili - damu- matapishi na mate - inaamanisha watu wanao wahudumia waathirika wamo katika hatari hata nao kuambukizwa.
Imegunduliwa pia katika shahawa ya wanaume walioponea na WHO linasema jitihada za kitaifa na kimataifa ni lazima zishinikizwe kuhakikisha wanaume hao wanakaguliwa shahawa zao kutambua iwapo wana uwezo wa kusambaza tena ugonjwa huo.
Na kazi lazima iendelee kutumia chanjo ya Ebola kwa watu walio karibu na waathiriwa walioponea ambao bado wanabeba virusi hivyo, Limesema WHO.
Lakini hakupaswi kuwa na vikwazo vya usafiri na biashara na Guinea, Liberia na Sierra Leone - hatua zozote kama hizo zinapaswa kuondolewa, limesema shirika hilo la afya duniani.
No comments:
Post a Comment