Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Wednesday, April 6, 2016

Ted Cruz amshinda Trump mchujo Wisconsin


TrumpImage copyrightGetty
Image captionCruz ameshinda upande wa Republican, naye Sanders akashinda Democratic
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Ted Cruz ameshinda mchujo wa chama hicho katika jimbo la Wisconsin, hilo likiwa pigo kubwa kwa Donald Trump.
Katika chama cha Democratic, Bernie Sanders alipata ushindi mkubwa dhidi ya Hillary Clinton anayeongoza kwa wajumbe kwa sasa.
Bw Trump anaongoza kwa wajumbe na katika kura za maoni chama cha Republican, lakini kuna wasiwasi kwamba huenda akashindwa kupata wajumbe wa kumuwezesha kuidhinishwa moja kwa moja kuwa mgombea.
Wapinzani wa Bw Trump wanatumai kwamba hilo likifanyika basi wanaweza kubadilisha mambo katika mkutano mkuu wa chama hicho wa kuidhinisha wagombea mwezi Julai.
Katika mkutano huo, iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya nusu ya wajumbe, ni viongozi wa chama ambao watakuwa na usemi katika kuamua mgombea.
“Leo ni siku muhimu sana, inatoa ujumbe kwa watu wa Marekani,” Bw Cruz amewaambia wafuasi wa chama hicho Milwaukee.
“Tunashinda kwa sababu tunaunganisha chama cha Republican.”
Bw Cruz huenda asipate wajumbe wa kutosha kumuwezesha kushinda uteuzi moja kwa moja, lakini viongozi wa chama cha Republican wanamuunga mkono katika juhudi za kumzima Bw Trump.
Image copyrightReuters
Bw Trump kwa upande wake amesema kwamba ana matumaini kwamba atafanikiwa licha ya kushindwa Wisconsin na akamshambulia mpinzani wake.
"Ted Cruz ni mbaya kushinda kikaragozi, yeye ni kama kirusi, anatumiwa na viongozi wa chama kutupokonya uteuzi,” maafisa wa kampeni wa Bw Trump wamesema kupitia taarifa.
Viongozi wa chama wana wasiwasi kwamba Bw Trump hatakuwa na nguvu sana katika kukabiliana na mgombea wa Democratic uchaguzini iwapo ataidhinishwa na pia kwamba anaweza kuathiri wagombea ubunge wa Republican uchaguzini.
Kura za maoni zinaonesha hapendwi na wanawake, watu wa Hispania na vijana.
Katika upande wa Democratic, ushindi wa Sanders jimbo la Wisconsin umemuongezea nguvu kabla ya mchujo muhimu New York na Pennsylvania.
DemocraticImage copyrightAP
Image captionSanders na Clinton ndio pekee waliosalia chama cha Democratic
Seneta huyo wa Vermont, akiwahutubia wafuasi wake Wyoming, amesisitiza kwamba kampeni yake inaendelea kushika kasi na kwamba atabadilisha mambo.
"Mabadiliko kamili huwa hayafanyiki kutoka juu kwenda chini, huwa yanatoka chini kwenda juu,” amesema.
Bi Clinton yuko mbele sana kwa wajumbe na wadadisi wengi wa kisiasa wanasema ana uwezekano mkubwa wa kushinda uteuzi wa chama cha Democratic licha ya kushindwa majimbo kadha karibuni.
Ingawa Bw Trump alishindwa mchujo huo wa Jumanne Wisconsin, bado ana muda wa kujikwamua.

Tuesday, April 5, 2016

Donald Trump amtaka Kasich kujiondoa


Image copyrightGetty
Image captionDonald Trump

Mgombea wa chama cha Republican aliiye kifua mbele Donald Trump amesema kuwa atashinda kwa urahisi uteuzi wa chama cha Republican iwapo John Kasich atajiondoa katika kinyang'anyiro hicho.
Amesema kwamba gavana huyo wa Ohio hafai kuendelea katika mchujo huo kwa kuwa hawezi kupata wajumbe wa kutosha ili kuweza kushinda.
Matamshi yake yanajiri wakati ambapo kura ya mchujo wa jimbo la Wisconsin inatarajiwa kutoa mwelekeo wa kinyang'anyiro hicho.
''Kama kusengekuwa na Kasich ,ningeshnda mara moja'',alisema Trump katika mkutano wake wa kampeni huko Wisconsin.
Iwapo bwana Trump atashindwa katika mchujo huo siku ya Jumanne kama inavyoonekana hakuna uwezekano kwamba atapata wajumbe 1,237 wanaotakikana kupata ushindi wa tiketi hiyo.
Wajumbe wanawakilisha majimbo katika mkutano wa vyama na huongezwa na kura katika kila jimbo.

Image copyrightReuters
Image captionJohn Kasich

Kufikia sasa Bwana Trump ana wajumbe 735, Seneta wa Texas Ted Cruz ana 461 naye Gavana wa Ohio bwana Kasich ana wajumbe 143.
Iwapo hakuna atakayefikisha wajumbe 1,237 baada ya majimbo yote 50 kupiga kura,basi huenda chama cha Republican kikapiga kura ,hatua inayomaanisha kwamba wajumbe watampigia kura wanayemtaka na huenda bwana Trump ambaye hapendwi na chama hicho akapoteza.

Saturday, April 2, 2016

Kukubaliana Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na uamuzi wa Mahakama ya Katiba


Kukubaliana Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na uamuzi wa Mahakama ya Katiba
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza kuwa, anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Kati ya nchi hiyo dhidi yake.
Rais Zuma alitangaza jana kwamba, anaheshimu uamuzi huo wa mahakama na kwamba, atarejesha katika hazina ya serikali kiasi cha fedha alichotakiwa kukirejesha baada ya kutumia fedha hizo katika mambo yake binafsi. Rais Zuma amesema kuwa, hakukiuka katiba ya nchi kwa makusudi. Rais huyo amesema kuwa, anaomba radhi yeye na kwa niaba ya serikali anawaomba radhi wananchi wa nchi hiyo na anavitaka vyama vyote vya kisiasa kuheshimu katiba.
Kwa mujibu wa uamuzi huo, Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini imemuagiza Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo kuirejeshea serikali fedhai zilizotumika kukarabati makazi yake binafsi, kwenye moja ya kashfa kubwa za ufisadi zilizowahi kuripotiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni. Hatua ya Rais Zuma ya kukarabati makazi yake binafsi kwa bajeti ya serikali, ni jambo ambalo lililipua ghadhabu za wapinzani na kuwakasirisha akthari ya wananchi wa nchi hiyo.
Chama kikuu cha upinzani katika Bunge la Afrika Kusini kimetangaza kuwa, kitatumia kila njia kuhakikisha Zuma anavuliwa madarakani endapo Bunge litazembea kufanya hivyo. Wabunge wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance (DA) wametangaza kuwa, wana mpango wa kuwasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo wa kutokuwa na imani na uwezo wa kisiasa wa Rais Zuma.
Jacob Zuma alishika hatamu za uongozi nchini Afrika mwaka 2009 katika hali ambayo, kabla ya kuchukua wadhifa huo, mahakama ilikuwa imemfutia tuhuma 700 za ufisadi wa fedha. Mwaka 2014 alifanikiwa kutetea kiti chake na hivyo kuongoza kwa muhula wa pili. Suala la ufisadi na ubadhirifu wa mali ni tatizo sugu katika nchi nyingi za Kiafrika na na viongozi serikali ndio watuhimiwa wakuu. Afrika Kusini nayo kwa mujibu wa asasi za kimataifa ni miongoni mwa nchi ambazo zinaongoza kwa visa vya ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma barani Afrika. Hii ni katika hali ambayo, hali mbaya ya uchumi imewafanya wananchi wa nchi hiyo walemewe na mzigo wa mashinikizo ya kifedha na akthari ya wananchi wanalalamikia jambo hilo. Hivi karibuni Rais Jacob Zuma alitangaza nia ya serikali ya kupunguza matumizi ya serikali. Aidha aliahidi katika mkutano wa kiuchumi wa Afrika kupambana na ufisadi wa fedha.
Licha ya kuwa katika miaka ya hivi karibuni, Afrika Kusini imekuwa ikipiga hatua katika ustawi wa kiuchumi, lakini matatizo ya kisiasa na migogoro kama ya nishati ya umeme na ukame ni mambo ambayo yametoa pigo kwa uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hiyo. Janga la ukame limepelekea kusimama mwenendo wa ukuaji wa uchumi nchini Afrika Kusini katika miezi mitatu ya mwisho mwa mwaka jana.
Aidha kiwango cha ukosefu wa ajira kimefikia asilimia 25 na kuongezeka idadi ya watu nchini humo walioambukizwa virusi vya ukimwi ni matatizo mengine yanayotajwa na wachambuzi wa mambo kwamba, yameyafanya maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu. Filihali, mazingira magumu ya kiuchumi kwa upande mmoja na suala la viongozi kutumia fedha za umma kwa masuala yao binafsi kwa upande wa pili, ni mambo ambayo yamelipua ghadhabu za vyama na wananchi wa nchi hiyo. Inaonekana kuwa, ahadi ya Rais Zuma ya kurejesha fedha kama alivyotakiwa na mahakama na kusisitiza kufungamana kwake na sheria ni hatua ambayo inalenga kupunguza makali ya mgogoro wa sasa wa nchi hiyo.

Thursday, March 31, 2016

DRC: Moïse Katumbi atawazwa kuwa "mgombea wa urais"


Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga Moïse Katumbi katika mahojiano mjini Lubumbashi, Juni 2, 2015.
AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kamati kuu ya muungano wa vyama 7 vya upinzani G7 imemteua rasmi Jumatano hii mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga, Moïse Katumbi kuwa mgombea katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya muungano huo.

Vyama hivi vilioondolewa hivi karibuni katika muungano unaounga mkono chama tawala cha PPRD.
Bila ubishi wowote, Moïse Katumbi ameteuliwa rasmi kuwa mgombea wa G7 katika uchaguzi wa urais utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Novemba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Tangazo hili limetolewa Jumatano Machi 30 baada ya mkutano wa kamati kuu ya muungano unaojumuisha vya saba vya upinzani vilioondolea serikalini, uliofanyika mjini Kinshasa. Vyama hivi viliondolewa katika muungano wa vyama vinavyokiunga mkono chama tawala cha PPRD, baada ya kuonyesha msimamo wao wa kupinga muhula wa tatu wa rais Joseph Kabila.
G7 imemuomba Moïse Katumbi kushiriki uchaguzi wa urais ambao umepangwa kufanyika Novemba 27.
Siku moja kabla ya uteuzi huo, mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga alikua amesha jiandaa kuwania katika kinyang'anyiro hicho, ambapo alikemea vikali mjini Lubumbashi, kusini mwa nchi hiyo "uchaguzi wa Wakuu wa Mikoa" ambao aliutaja kuwa "uligubikwa na kasoro nyingi".
Hata hivyo Katika mkoa huo mpya wa Katanga, muungano wa vyama vilio serikalini vilipata ushindi katika uchaguzi wa wakuu wa Mikoa uliofanyika Machi 26, huku wagombe wa muungano wa G7 wakibatilishwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kwa "ombi la moja kwa moja" la muungano wa vyama vilio serikalini, jambo ambalo Moïse Katumbi, alikemea pia, akibaini kwamba hiyo ni moja ya dalili zinazoonyesha "jinsi gani sheria zinadidimizwa na demokrasia kotoendelea nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo".

Chama kikubwa cha kisiasa Brazil chajiondoa serikalini

Serikali ya Brazil imepata pigo baada ya chama mshirika cha PMDB, kujiondoa katika serikali ya muungano, kikisema kimeacha kuiunga mkono serikali ya Rais Dilma Rousseff.
Chama cha Democratic Movement-PMDB ambacho ni chama kikubwa cha kisiasa nchini Brazil, kimetangaza kujiondoa kwenye serikali ya muungano ya Rousseff kwa kuwataka mawaziri wake sita wajiuzulu mara moja au wachunguzwe na kamati ya maadili ya chama hicho. Makamu rais wa chama hicho, Seneta Romero Juca, mwenye ushawishi mkubwa, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya wabunge 100 kuidhinisha uamuzi huo.
''Kuanzia leo na kuendelea katika mkutano huu wa kihistoria wa PMDB, chama chetu kinajiondoa kwenye serikali ya Rais Dilma Rousseff na hakuna hata mtu mmoja anayeruhusiwa kushika wadhifa wowote wa shirikisho chini ya jina la chama chetu,'' alisema Juca.
Mkutano wa chama cha PMDB
Mkutano wa chama cha PMDB
Kujiondoa kwa chama hicho sasa kunamuweka mahali pabaya Rais Rousseff katika hatari ya kuondolewa madarakani na bunge. Hali hiyo inaondoa nafasi ya kiongozi huyo kupata theluthi moja ya kura za bunge ambazo anazihitaji kujitetea asiondolewe madarakani katika kura ya kutokuwa na imani naye, inayotarajiwa kupigwa mwezi ujao wa Aprili.
Mkutano wa chama hicho ulimalizika huku ukikitaka chama cha Wafanyakazi cha kiongozi huyo kuondoka madarakani na Makamu wa Rais wa Brazil, Michel Temer, ambaye ni wa chama cha PMDB, awe rais mpya.
Temer anaendelea kuwa makamu wa rais
Temer mwenye umri wa miaka 75, ambaye anaendelea kuwa makamu wa rais chini ya serikali ya sasa ya Brazil licha ya kuvunjika kwa serikali ya muungano, atakuwa rais wa mpito iwapo Rais Rousseff ataondolewa madarakani na bunge.
Aidha, hatua hiyo imemfanya kiongozi huyo kuahirisha ziara yake nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa kilele wa usalama wa nyuklia utakaofanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa, ili aweze kukabiliana na mzozo unaoendelea nchini kwake ambao unatishia kumuondoa katika nafasi yake.
Utafiti wa maoni uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa asilimia 68 ya watu wanawataka wabunge wapige kura ya kutokuwa na imani na Rais Rousseff, huku asilimia 11 tu wakiamini kwamba watakuwa na serikali bora chini ya Temer.
Maandamano ya kumpinga Rais Dilma Roussef
Maandamano ya kumpinga Rais Dilma Roussef
Wananchi wa Brazil wamekuwa katika maandamano makubwa wakimshinikiza Rais Rousseff ajiuzulu kutokana na kashfa kubwa ya rushwa dhidi ya kampuni ya mafuta ya Petrobras. Wafuasi wa rais huyo wamesema maandamano ya kumtaka ajiuzulu ni sehemu ya jaribio la mapinduzi na wameapa kuandamana pia kuutetea utawala wake.
Hivi karibuni jaji mkuu wa Brazil, alipitisha uamuzi kumzuia rais wa zamani wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva kuchukua wadhifa wake kama mnadhimu mkuu wa baraza la mawaziri. Wakosoaji wanasema hatua ya Rousseff kumteua Lula, ni jaribio la kumkinga dhidi ya kashfa ya rushwa inayomkabili.

Wednesday, March 30, 2016

Hotuba ya Trump yatumiwa katika filamu


Image copyrightReuters
Image captionDonald Trump
Wazalishaji wa filamu moja nchini Mexico kuhusu wahamiaji wanaojaribu kuingia nchini Marekani wametoa kipande kidogo cha filamu hiyo ambacho kinatumia hotuba ya bwana Donald Trump kupitisha ujumbe wa filamu hiyo kwamba maneno ni hatari kama risasi.
Sauti iliowekwa katika filamu hiyo ya Kihispania, Desierto ,inemuonyesha bwana Trump akiitaka Mexico kusitisha kuwaingiza Marekani walanguzi wa dawa za kulevya pamoja na walanguzi wa binaadamu haraka iwezekanavyo.
Kipande hicho cha filamu kinaisha na mlinzi mmoja akiwawinda wahamiaji jangwani.Filamu hiyo inaigizwa na Garcia Gael Bernal na inaelekezwa na Jonas Cuaron ,mwanawe mwelekezi aliyeshinda tuzo za Oscar Alfonso Cuaron

Trump amtetea meneja wake aliyeshtakiwa


LewandowskiImage copyrightReuters
Image captionBw Lewandowski akiwa na Bw Trump
Mgombea urais anayeongoza katika chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemtetea meneja wake wa kampeni ambaye ameshtakiwa kumdhulumu mwanahabari wa kike.
Bw Corey Lewandowski tayari ameshtakiwa, na duru zinasema anapanga kukanusha mashtaka hayo. Akiongea na wanahabari, Bw Trump ametoa wito kwa Bw Lewandowski kutokubali kutatua kesi hiyo na Michelle Fields nje ya mahakama.
Kanda ya video iliyotolewa na maafisa wa polisi inamuonesha Bw Lewandowski akimvuta mwanahabari huyo na kumuondoa karibu na Bw Trump mwanahabari huyo alipojaribu kumuendea mgombea huyo wa urais katika kikao na wanahabari jimbo la Florida akitaka kumuuliza swali.
LewandowskiImage copyrightGetty
Image captionBw Lewandowski anapanga kukanusha mashtaka
Polisi wamemfungulia Bw Lewandowski mashtaka ya kumshambulia mwanahabari huyo, wakisema alimuumiza mkono.
Bw Trump amesema huo ni ukiukaji wa haki akisema polisi hawakumhoji Bw Lewandowski wakati huo.
Mgombea urais anayeshindana na Bw Trump, Ted Cruz, amesema kisa hicho ni ishara tu ya utamaduni wa dhuluma ambao umo kwenye kampeni ya Bw Trump.

Tuesday, March 29, 2016

Uchaguzi wa Zanzibar waikosesha hela Tanzania


Uchaguzi
Image captionMwanamke akipiga kura wakati wa uchaguzi Zanzibar
Shirika la ufadhili la serikali ya Marekani limesitisha ufadhili wake kwa serikali ya Tanzania likilalamikia matukio kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea ufadhili wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni sawa na shilingi trilioni moja za Tanzania.
Kupitia taarifa, bodi hiyo imesema: "Serikali ya Tanzania haijachukua hatua za kuhakikisha kuheshimiwa kwa uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao.”
Bodi hiyo aidha imesema Tanzania iliendelea na uchaguzi wa marudio Zanzibar ambao "haukujumuisha wote na wala haukuakisi maoni ya wote, licha ya malalamiko kutoka kwa serikali ya Marekani na jamii ya kimataifa.”
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt Ali Mohammed Shein alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo uliosusiwa na chama kikuu cha upinzani, Chama cha Wananchi (CUF).
MCC imesema kwamba huwa inatilia mkazo sana demokrasia na kujitolea kwa nchi kufanikisha uchaguzi huru na wa haki.
"Uchaguzi uliofanyika Zanzibar na kutekelezwa nwa Sheria ya Uhalifu wa Mitandao vinaenda kinyume na hili,” imesema.
Tanzania ilipokea Dola 698 milioni katika awamu ya kwanza.

FREEMAN MBOWE: CCM WAJIPANGE UCHAGUZI UJAO

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, amewashauri Watanzania wasife moyo kwa matokeo mabaya ya uchaguzi yaliyopinduliwa, na kuongeza kuwa matokeo hayo yawe chachu ya kufanya vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.

Mbowe ameeleza kuwa uchaguzi sio tukio, bali mchakato, hivyo kama kuna watu wamekufa moyo kwa sababu ya kilichofanywa na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupindua matokeo, hasa ya urais, watafakari upya na wajipange kwa kazi kubwa inayokuja, kwani mafanikio ya kisiasa hayapimwi kwa tukio moja la uchaguzi.

Mbowe amesema hayo Masaki jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa Zamani ambaye pia alikuwa Mgombea Urais wa Chadema aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwenye hafla ya kumshukuru Mungu iliyoandaliwa na familia hiyo. Ukawa unaundwa na Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

“Hatukushinda serikali kuu kama tulivyokusudia na kupenda iwe kwa sababu ambazo si wakati wake kuzisema sasa, lakini ni vyema tukumbuke kwamba mapambano tunayofanya, kama kuna yeyote miongoni mwetu anafanya kwa ajili yake binafsi, ana wajibu wa kujitafakari upya,” amesema Mbowe.

Monday, March 28, 2016

Trump aikosoa jumuiya ya kujihami ya NATO


Trump anayewania uteuzi wa chama cha Republican kugombea urais wa Marekani (08.11.2016) amependekeza kuziachia Japan na Korea Kusini zitengeneze silaha za nyuklia kujilinda dhidi ya Korea Kaskazini na China.
USA Vorwahlen in Florida Donald Trump in West Palm Beach
Bilionea Donald Trump akiwa West Palm Beach, Florida (15.03.2016)
Trump alisema muungano wa kijeshi wa NATO umepitwa na wakati na kupendekeza ufanyiwe mageuzi. Trump pia alisema jumuiya ya NATO yenye nchi 28 wanachama iliundwa wakati wa enzi tofauti wakati kitisho kikubwa kwa nchi za magharibi kilikuwa ni muungano wa zamani wa Sovieti. "NATO haina uwezo wa kupambana na ugaidi na inaigharimu Marekani fedha nyingi mno," akaongeza kusema mgombea huyo.
Kauli hiyo ameitoa siku chache kabla kufanyika mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia mjini Washington kuhusu usalama wa silaha za nyuklia. Rais wa Marakani Barack Obama atauandaa mkutano huo siku ya Alhamisi na Ijumaa wiki hii utakaowaleta pamoja wajumbe 56. Huku mkutano huo ukitarajiwa kujikita katika kutafuta njia za kuepusha mashambulizi ya kigaidi dhidi ya vituo vya nykulia, mapendekezo ya Trump huenda yakajadiliwa pia, hususan pembezoni mwa mkutano. Urusi haitahudhuria mkutano wa mjini Washington, lakini rais wa China, Xi Jinping atahudhuria.
Machi 21 mwaka huu Trump alisema Marekani inatakiwa ipunguze ufadhili wake kifedha kwa NATO, iliyoundwa mwaka 1949 baada ya vita vikuu vya pili vya dunia na kuwa ukuta wa ulinzi dhidi ya utanuzi wa muungano wa Sovieti.
Mgombea hasimu wa Trump kwa uteuzi wa chama cha Republican seneta wa jimbo la Texas, Ted Cruz, aliyaeleza maoni ya Trump kuhusu NATO kuwa ya kipuuzi. Cruz alisema kuliacha bara la Ulaya, kujiondoa kutoka kwa muungano uliofanikiwa zaidi katika nyakati za sasa, hakuna maana yoyote, akiongeza kuwa kufanya hivyo kutampa ushindi mkubwa rais wa Urusi, Vladimir Putin, na kundi la Dola la Kiislamu IS.
Katika hatua nyingine inayoondokana kabisa na sera ya kihistoria ya Marekani, Trump alisema katika mahojiano yaliyochapishwa jana na gazeti la New York Times kwamba atazingatia kuiachia Japan na Korea Kusini zitengeneze silaha zao za nyuklia, badala ya kuitegemea Marekani izilinde kutokana na kitisho cha Korea Kaskazini na China.
Trump kuziruhusu Japan na Korea Kusini kwa na nyuklia
Katika mahojiano hayo Trump alisema atakuwa tayari kuwaondoa wanajeshi wa Marekani kutoka Japan na Korea Kusini mpaka nchi hizo mbili zilipe fedha zaidi kuwahudumia na kuwalisha. Marekani ina wanajeshi 50,000 nchini Japan na wengine 28,500 nchini Korea Kusini.
Waziri kiongozi wa Japan, Yoshihide Suga, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari leo mjini Tokyo kwamba hakujafanyika mageuzi ya sera ya Japan ya kutojenga, kumiliki au kuanzisha silaha za nyuklia na akasisitiza bila kujali nani atakayekuwa rais wa Marekani, uhusiano kati ya Marekani na Japan utaendelea kubakia kuwa msingi imara wa diplomasia ya Japan na muhimu kwa uthabiti wa kanda hiyo na dunia kwa ujumla.
Trump, mfanyabiashara bilionea kutoka New York anayetaka ateuliwe na chama chake cha Republican kugombea urais wa Marekani katika uchaguzi wa Novemba 8 pia alisema huenda akasitisha ununuzi wa mafuta kutoka kwa Saudi Arabia na mataifa mengine ya kiarabu yaliyo washirika wake hadi pale yatakapotoa wanajeshi wa ardhini kupambana na kundi la dola la kiislamu au yailipe Marekani kwa kufanya hivyo.

Mvutano katika uhusiano wa Rwanda na Burundi


Mvutano katika uhusiano wa Rwanda na Burundi
Chama tawala Burundi kimemtuhumu Rais wa Rwanda kuwa anatekeleza maangamizi ya kizazi. Paschal Nyabenda mkuu wa chama tawala cha Burundi CNDD-FDD ameashiria maangamizi ya kizazi yaliyojiri Rwanda na kueleza kuwa Rais Paul Kagame wa nchi hiyo anawasajili vijana wa Burundi katika kambi za wakimbizi zilizopo Rwanda na kuwapatia mafunzo, ili baadaye wakirejea nchini kwao watekeleze mauaji ya kimbari.
Mkuu wa chama tawala nchini Burundi pia amezituhumu baadhi ya serikali za Ulaya kuwa zinampatia silaha na fedha Rais wa Rwanda kwa lengo hilo hilo. Hii ni mara nyingine ambapo Burundi inaituhumu Rwanda kuwa inawapa mafunzo ya kijeshi wakimbizi wa nchi hiyo ili baadaye wakirudi Burundi watekeleze oparesheni za kijeshi.
Raia wa Burundi zaidi ya laki mbili na nusu wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Rwanda, kufuatia kupamba moto hali ya mchafukoge na mivutano ya kisiasa nchini Burundi. Serikali ya Bujumbura inawatuhumu vioongozi wa serikali ya Rwanda, khususan Rais Rais Paul Kagame mwenyewe kuwa wanaingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo na kufanya kila wawezalo ili kumuondoa madarakani Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi.
Kabla ya hapo na baada ya serikali ya Burundi kutoa madai hayo, Umoja wa Mataifa uliamua kutuma ujumbe wa wataalamu wake nchini humo ili kufanya uchunguzi zaidi. Uchunguzi huo umethibitisha suala hilo, hata hivyo viongozi wa Rwanda wameutaja utafiti huo kuwa ni wa uwongo.
Siku kadhaa zilizopita pia Wizara ya Mambo ya Ndani na Masuala ya Uzalendo ya Burundi ilitangaza kuwa inajiandaa kufungua mashtaka dhidi ya serikali ya Rwanda na Rais Paul Kagame wa nchi hiyo ambayo yatawasilishwa kwa taasisi za kisheria za kimataifa.
Mapigano nchini Burundi yalianza mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka jana kufuatia hatua ya Pierre Nkurunziza ya kugombea tena kiti cha urais kwa muhula wa tatu. Licha ya kutekelezwa jitihada za kimataifa kwa minajii ya kuhitimisha mgogoro owa Burundi, lakini juhudi hizo hadi sasa zimeshindwa kuzaa matunda. Benjamin Mkapa Rais mstaafu wa Tanzania siku kumi zilizopita alielekea Burundi akiwa kama mkuu wa kundi la usuluhishi katika mgogoro wa nchi hiyo na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza. Baada ya mazungumzo hayo, Mkapa alisema kuwa anataraji kwamba machafuko na mzozo wa ndani unaoikabili Burundi utapatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Kabla ya kufanya mazungumzo na Rais wa Burundi, mkuu wa kundi la usuluhishi katika mzozo wa Burundi alikuwa ameshafanya mazungumzo pia na Marais wa Uganda na Rwanda.
Benjamin Mkapa amesema kuhusiana na hitilafu kati ya Burundi na Rwanda kuwa, nchi za Kiafrika ni wanachama wa taasisi moja, na kwamba nchi hizo zikiwa majirani zinapaswa kushirikiana na kuishi katika mazingira ya amani, utulivu ili kuimarisha ustawi wa kiuchumi kwa pamoja.
Wakati huo huo machafuko nchini Burundi yangali yanaendelea. Siku chache zilizopita miripuko kadhaa ilitokea katika maeneo tofauti nchini humo na kuuwa na kujeruhi watu kadhaa. Naibu Msemaji wa polisi ya Burundi juzi alitangaza kuwa wanajeshi wanne wa nchi hiyo walishambuliwa na kujeruhiwa na watu waliokuwa na silaha wakati wanajeshi hao walipokuwa kwenye doria katika eneo la Musaga kusini mwa Bujumbura mji mkuu wa Burundi. Aidha watu wasiopungua watatu walijeruhiwa katika miripuko miwili ya guruneti huko Mutanga kaskazini mashariki mwa Bujumbura. Miripuko hiyo imetekelezwa siku mbili baada ya kuuliwa Darius Ikurakure na Didier Muhimpundu maafisa wawili wa jeshi la Burundi.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita liliitisha kikao kujadili hali ya mambo ya Burundi. Katika kikao hicho, taasisi zisizo za kiserikali za nchi wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ziliitaka serikali ya Burundi ianzishishe mchakato wa mazungumzo ya kisiasa kati yake na wapinzani.