Janet Museven Waziri wa Elimu wa Uganda na mke wa raisi Yoweri Museven
Uganda inamshikilia
mwanaharakati na muhadhiri wa chuo kikuu cha Makerere kwa kumkosoa mke
wa raisi wa Uganda kupitia mtandao wa kijamii.
Stella Nyanzi alimkosoa Bi Janet
Museveni, ambaye ni waziri wa elimu kupitia ukurasa wake wa face book
baada ya serikali kusema inaandaa mpango wa kugawa taulo za kike kwa
wasichana wanafunzi ambao wapo katika mazingira magumu ya kupata vifaa
hivyo.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima amethibitisha kukamatwa kwa Stela Nyanzi ambaye atafikishwa mahakamani siku ya jumatatu jijini kampala kwa matumizi mabaya ya mtandao na kuvunja sheria ya mawasiliano ya mwaka 2011.
Kwa mujibu wa Kayima Bi Stella Nyanzi amekuwa akichapisha masuala yanayotazamwa kama vita kupitia mtandao wa kijamii ambayo hayana maslahi kwa taifa.

No comments:
Post a Comment