Chama cha wamiliki wa Mabasi (TABOA) na wamiliki wa malori na Chama
cha wasafirishaji kimetangaza kwa pamoja mgomo wa usafirishaji abiria na
mizigo nchi nzima.
Uamuzi huo umefanyika kwa ushirikiano wa vyama vyote vitatu Dar es
Salaam kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha
sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa
siku ya Jumanne wiki ijayo.
Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutano mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Eneo Mrutu amesema sheria inayolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva kusababisha mmiliki kufungwa jela.
Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.
" kinachosababisha mgomo wa wamiliki ni majukumu mapya kwa wasafirishaji chini ya kanuni mpya za Sumatra," baadhi ya wadau wameeleza hilo.
Wamesema kuwa majukumu haya yanapatikana katika rasimu ya Kanuni mpya za Usafirishaji Abiria Kifungu cha 21: Wajibu wa mmiliki/mwenye leseni na mtoa huduma.

No comments:
Post a Comment