Kiungo wa Yanga raia wa Rwanda Haruna Niyonzima ambaye pia ni
nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema, katika soka la kisasa maandalizi
ndio kilakitu katika kuhakikisha timu inapata matokeo na sio kubadili
uwanja.
Hivi karibuni Yanga iliwasilisha maombi shirikisho la soka Afrika CAF
ili mechi yao ya nyumbani ya mchujo kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya
makundi ya kombe ka shirikisho barani Afrika ichezwe kwenye uwanja wa
CCM Kirumba Mwanza badala ya uwanja wa taifa. Maombi hayo hayakufanikiwa
baada ya uwanja wa CCM Kirumba kutokidhi viwango vya CAF na kutakiwa
kufanyiwa marekebisho ambayo hayawezi kukamilika ndani ya muda kabla ya
mechi hiyo.
“Ukijiandaa vizuri haijalishi uwanja, Mwanza sio mbali mashabiki
wanasafiri hadi nje ya nchi sasa Mwanza watashindwaje kwenda kwa hiyo
presha ambayo tunaipata hapa haitakuwa tofauti sana na ya Mwanza kwa
sababu ni Tanzania ileile.”
“Kwa upande wangu haina haja kubadili uwanja kwa sababu mpira unaweza
kuchezeka sehemu yoyote. Sidhani hata kama walimu walipendekeza hivyo,
itakuwa ni wadau lakini mpira wa kisasa hauko hivyo, sehemu yoyote
unacheza mpira inategemea na wewe ulivyojiandaa.”
Kwa maana hiyo, Yanga itacheza mechi yake dhidi ya MC Algers kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam na si vinginevyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment