Na Zainabu Rajabu
MOJA ya sababu inayomfanya kiungo wa Mwadui FC ya Shinyanga Hassan
Kabunda kucheza soka kwa kujituma ni kutafuta pesa kwa ajili ya
kumsaidia mdogo wake kike ambaye ni mlemavu na anamtegemea kwa sasa.
Tangu Kabunda asajiliwe na Mwadui FC ya Shinyanga akitokea timu ya
Asanti United ya ligi daraja la kwanza, amekuwa na msimu mzuri katika
ligi kuu na kufanikiwa kutikisa nyavu mara 6.
Shaffihdauda.co.tz. ilimtembelea Hassan Kabunda nyumbani kwao na
kupiga nae stori kadhaa kuhusiana na maisha yake ya soka ambapo alisema:
“Nimekuwa najituma na kupambana katika maisha yangu ili niweze kumpa
maisha mazuri dada yangu kipenzi Noun Kabunda ambaye amekuwa ndiyo
furaha yangu pale ninapo muona akitabasamu.”
“Ninapo muangalia dada yangu katika hali aliyonayo naumia sana lakini
huwezi kumkufuru Mwenyenzi Mungua kwa livyomuumba, napambana ili niweze
kumtimiza mahitaji yake nikiwa kama kaka mkubwa.”
Kinda huyo amesema, amekuwa akivutiwa na uchezaji wa Farid Mussa
anaekipiga katika timu ya Tenerife ya nchini Hispania, huku akisema ni
mchezaji ambaye anaweza kujilinganisha nae kutokana na kwamba wote
wanacheza katika nafasi inayofana.
Mdogo wake Kabunda ana ulemavu wa viungo ambao alizaliwa nao na kaka
yake (Hassan Kabunda) anapambana kwenye soka ili kupata pesa za kuweza
kumtunza na kumpatia mahitaji muhimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment