Baada ya Simba kupoteza mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara
dhidi ya Kagera Sugar kwa kuchapwa 2-1, nahodha wa Simba Jonas Mkude
amesema bado wanaendelea kufukuzia ubingwa hadi mwisho kwa sababu bado
ipo nafasi ya kushinda taji hilo ikiwa watafanya vizuri kwenye mechi zao
zilizosalia kwenye ratiba ya ligi.
“Ndiyo matokeo ya mchezo, tumepoteza mechi lakini bado hatukati tama,
tutapambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda ubingwa wa ligi,”
alisema Mkude mara baada ya mchezo wakati akizungumza na Azam TV.
“Nafasi bado ipo, sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu mbili
zilizobaki huku Kanda ya Ziwa. Mashabiki waendelee kutuunga mkono wasife
moyo bado tupo kwenye nafasi nzuri.”
Simba ina mechi mbili dhidi ya timu za mkoa wa mwanza (Toto Afrikans
na Mabao FC)ambazo zote zinapambana kukwepa mkasi wa kushuka daraja
hivyo Wekundu wa Msimbazi watakutana na upinzani mkali kutoka kwa timu
hizo huku Toto Africans ikiwa na historia nzuri kuifunga Simba kwenye
mechi za ligi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment