
Mamlaka ya jeshi la
Colombia inasema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini
humo imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.
Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana . Vikosi vya wafanyikazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wanasema nyingi ya barabara za kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa hazipitiki kutokana na mkasa huo.

Viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.
Rais Juan Manuel Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokoaji.

Maporomo koya ardhi yamekumba eneo hilo mara kadha miezi ya hivi karibuni.
Mwezi Novemba, watu 9 waliuawa kwenye mji wa El Tambo, karibu kilomita 140 kutoka Mocoa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababiswa na mvua kubwa.

No comments:
Post a Comment