Showing posts with label MAUSIANO. Show all posts
Showing posts with label MAUSIANO. Show all posts

Wednesday, June 8, 2016

Matumizi Ya SMS 12 Za Kumsuka Mwanamke

Ok umefanya bidii umeapproach mwanamke kwa mbinu za kistadi ukafaulu kuiteka atenshen na hisia zake kwako.

Umeongea na yeye kwa masaa na ukatumia mbinu murua mpaka akakupatia namba yake ya simu.

Siku ya pili umeanza kuchat naye mpaka umemzoea, amekuzoea.

Imepita siku kadhaa bado mnatumiana jumbe fupi lakini inafika mahali flani unaona kama gemu yako inaenda kimtindo ambao hautarajii.

Unajaribu kutumia mbinu nyingine za kijanja lakini unaona kama jumbe zenu zinafifia.

Relax. NESIMAPENZI.com iko hapa.



Leo tumeamua kukuletea baadhi ya SMS unafaa kumtumia mwanamke kuyafanya maongezi yenu yawe ya kuvutia. Mwanzo nimekuchagulia baadhi ya SMS ambazo huzitumia binafsi wakati ambapo nacheza na jumbe kwa wanawake.

Zama nami.

SMS za kumtumia dem ili akupende zaidi

1. Ok tuseme unayechat na yeye ameangusha mstari wa kuchekesha. Badala ya wewe kujibu 'hahahah', unaweza kumjibu hivi:
Hahah! Njoo kwangu hii wikendi. Mimi ntaleta chakula wewe njoo na ucheshi wako.
ama
Hahah! Mbona hii wikendi tusiende kumtembelea John? Mimi ntaenda na chakula, wewe utakuja na ucheshi [Soma: Jinsi ya kufanya ili mwanamke akuachie namba yake ya simu mwenyewe]
2. Kama unayemzimia umekupa fununu ya kuwa ameboeka ama akikwambia ya kuwa hajafanya jambo la kumsisimua siku nzima unaweza kumjibu hivi:
Well, nlikuwa naenda matembezi sahizi kununua ice cream na vibanzi, wataka twende pamoja?
3. Kama unayempenda amekutumia meseji akikuambia ya kuwa amekumiss, ama alitamani ungekuwa katika mkutano flani ambao hukuwepo ungemjibu hivi:
Najua napendeka. Bila shaka najua pia mimi ningejimiss kama sikujiona katika huo mkutano :-)
4. Ukigundua kama mwanamke anakupenda halafu akakutext "hello, mambo vipi?" Unafaa kumjibu kwa kumthamini kujiona kama umempa kipao mbele. Waweza kumjibu hivi.
Hello mrembo. Nimetoka kwa mazoezi sahizi/gym...waweza kunipa muda kiasi nioge kabla sijarudi?
5. Jaribu kutumia jina la unayemzimia kila baada ya sms 4-5 hivi. Utakuwa unaigonga hisia yake.
Hi Mourine, usiniambie utakosa kuhudhuria. Utakosa mengi

Mambo Pete, wasemaje?
6. Kama umeona sms ambayo imekufurahisha ama kukuchekesha, huyo mwezako hawezi kuona. Hivyo lazima umjibu kwa mtindo flani kuashiria ya kuwa umefurahishwa. Mtumie meseji ya kuzidisha jambo.
Lol. Hahah umenichekesha karibu uvunje mbavu zangu. Hivi huu ucheshi wote unautoa wapi? [Soma: Sheria za kufuata wakati unapomtumia Sms mwanamke]
7. Wakati flani inaweza kutokea unayechat naye akakueleza mambo ambayo aliweza kufanya hadi akafanikiwa. Usipoteze nafasi hii nzuri ya kutoa pongezi yako kistadi
Wow! Niseme nimependezwa ama nimependezwa na wewe....chagua moja ;-)
8. Kama mazungumzo yenu yamefikia level ya tenshen ya kimapenzi unaweza kumtext hivi
Hivi usiku huu umevalia nini?

Eti wataka kuniambia umelalia tumbo lako ama mgongo wako?
9. Kama ni sms ya kwanza ya siku jaribu kuwa mfidhuli na msukaji wakati uo huo
Hello. Kwani wewe ni nani? Ama ni yule mwanamke mrembo niliyekuwa nikichat naye jana.
10. Kubadilisha gumzo ghalfa wataki ambapo mnarushiana sms za mapenzi
Wewe: Kabla hatujaendelea na chat, kuna kitu nataka kukuambia...pole.
Mwenza: Ok, niambie hakuna shida
Wewe: Siku ya kwanza nlipokutana na wewe nilivutiwa na wewe hapo hapo ;-)
11. Unaweza kumwitisha mwanamke mtoke out bila kuifanya ionekane kama ni deti
Wewe: So kawaida siku za wiki nyakati za jioni unafanya nini?
Mwenza: Nini nini nini
Wewe: Basi kesho naona utakuwa ukifanya jambo tofauti wakati huo
Mwenza: Kitu gani kimekufanya mpaka useme hivyo?
Wewe: Sababu kesho naja kukuchukua nikutembeze ulijue jiji. Tutapumzika kwa mkahawa flani mida ya saa tatu usiku...na tafadhali usiulize maswali ya zaidi. [Soma: Sms za kufanya maongezi yako na mwanamke yavutie]
12. Kama wewe na mwenza wako mnasoma ama mnafanya kazi sehemu moja unaweza kumtumia jumbe io hio siku baada ya nyinyi kufumukana.
Leo ulikuwa umevalia kunipendeza...ni ukweli ama nimekosea ;-)
Ok. Matumizi ya hizi sms zitalingana na wakati na jinsi ambavyo zinatumika. Huu ni mfano tu, unaweza kujeuza sms hizi ili zifanye kazi kwako. Usisahau kusoma machapisho ya awali tuliyoyachapisha ili unoe makali yako wakati wa kumtext mwanamke.

Monday, April 4, 2016

MAMBO YANAYOMFANYA MTU AYACHUKIE MAPENZI


MAMBO YANAYOMFANYA MTU AYACHUKIE MAPENZI
SIJUI wewe ulikuwa una malengo gani wakati unafikiria kuwa na ambaye unaye; wapo ambao walikuwa na malengo kwamba akiwa na mwanaume, maana yake awe ndio sawa na mashine ya kutolewa fedha maarufu kama ATM.

Ikiwa ulichokuwa unatafuta ni mwanaume au mwanamke ambaye kwako atakuwa ni ATM, kwamba ndiye awe anakupa kila kitu unachotaka, ikiwa hatakuwa na fedha si rahisi mkaendelea kuwa na uhusiano mzuri, kwa kuwa mpango wako haukuwa mapenzi, bali kuchuma fedha na kula raha.

Wajinga ni wale ambao wanaingia kwenye mapenzi ili kusaidiwa tu, badala ya kusaidiana. Mwenye hekima ni yule ambaye anafahamu kwamba kuingia kwenye mapenzi, maana yake ni kuongeza timu ya kusaidiana katika maisha, si vinginevyo.

Mwanamke yeyote ambaye anafikiri yuko na mwanaume maana yake ni kwamba awe anamnunulia kila kitu, kwamba kwake mwanaume ni kila kitu, kinywaji anunuliwe, chips anunuliwe nk…kwamba yeye ni mtu wa kupewa tu ofa, maana yake ni kwamba akili yake imekufa.

Kufikiri kwamba kuoana na fulani maana yake ni sasa yeye atakuwa anakusaidia kila kitu milele na kwamba asipofanya hivyo utamdharau, si kitu sahihi.

USIWE NA MATARAJIO MAKUBWA UNAPOINGIA KWENYE NDOA

Unapoingia kwenye ndoa, usiwe na matarajio makubwa sana mazuri. Jambo unalopaswa kufahamu ni kuwa uhusiano ni suala la kawaida, kwamba unakuwa na mtu kwa lengo la kuwa nae kama timu moja kusaidiana katika kuleta maendeleo.

Kati ya mambo yanayofanya watu kutofurahia mapenzi, ni pale anapotishwa kwamba labda asipofanya hiki kwa mfano kukusaidia, basi uhusiano wenu utaharibika.

Kuna wanawake utasikia aaah sasa kuna maana gani ya kuwa na mwanaume ikiwa namwomba fedha hawezi kunisaidia? Fikra kama hii ni ya kipuuzi. Wewe kwanini huna fedha? Ndoa ni kusaidiana, sio kugeuzana ATM.

YUKO BIZE NA SIMU, KOMPYUTA N.K

Kati ya mambo yenye kutiana ‘kichefuchefu’ katika mapenzi ni pale kwamba uko na mwenzi wako, lakini ni kama wewe ni tambala la deki; yaani yuko bize na simu yake au kompyuta au kitu kingine chochote.

Wengine unakuta labda anawasiliana na wengine kwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter nk, kumaanisha kwamba wewe ni muhimu, walio muhimu ni wale ambao anawasiliana nao huko.

KUKOSOANA MBELE ZA WATU AU HATA KUPIGANA

Wapo watu wamekuwa na tabia ya kukosoana au hata kupigana mbele za watu. Kati ya makosa yenye kukera na huenda ukasababisha uhusiano ukabaki historia ni hii…ni vizuri ndugu yangu kujifunza namna ya kuachana na hasira kali.

MATUMIZI MABAYA YA FEDHA NA KUTOKUWA NA MIKAKATI KATIKA MAISHA

Kila mtu Duniani anataka maisha bora, kwa maana hiyo ni furaha ya kila mtu kuona mwenzi wake anakuwa mwenye mikakati imara katika kuimarisha maisha yao. Tabia kama za ufujaji wa fedha, kutokuwa na mikakati katika maisha, ni kati ya mambo yanayochangia ndoa au uhusiano wa mapenzi kuwa mbaya.