Showing posts with label MAAJABU. Show all posts
Showing posts with label MAAJABU. Show all posts

Sunday, April 24, 2016

Jino kubwa la nyangumi lapatikana Australia

JinoImage copyrightAFPMuseum Victoria
Image captionJino hilo lilipatikana mwezi Februari
Jino kubwa la nyangumi limepatikana ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la kwanza kwamba nyangumi wakubwa hatari sana waliishi mbali na Amerika.
Mkusanyaji wa visukuku Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12) ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari.
Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi.
Inakadiriwa kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano iliyopita. Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani duniani.
Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".
NyangumiImage copyrightDominica Sperm Whale Project
Image captionNyangumi wakubwa baharini
Hadi kupatikana kwa jino hilo Beaumaris, visukuku vya nyangumi wakubwa vilikuwa vinapatikana pwani ya magharibi ya mabara ya Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.
Makavazi hiyo imesema nyangumi mwenye jino hilo huenda alikuwa na urefu wa mita 18 na uzani wa tani 40.

Tuesday, April 19, 2016

Kwa Picha: Baadhi ya vyoo bora zaidi duniani

Image copyright

Mwongozo wa vyoo 100 bora zaidi duniani umechapishwa na kampuni ya usafiri ya Lonely Planet.
Mwongozo huo umeorodhesha vyoo vya kila aina ambavyo bila shaka vina uwezo wa kuwaacha wasafiri vinywa wazi au kuwa na kumbukumbu za kusalia nazo daima.
“Vyoo ni dirisha la kuingia ndani katika moyo wa pahala Fulani. Isitoshe, bila kujali unavipa jina gani, vyoo huwaweka watu wote katika ngazi sawa,” kitabu hicho kinasema.
Hapa chini ni baadhi ya vyoo vilivyo kwenye mwongozo huo.
VyooImage copyrightALAMY
Vyoo hivi vinapatikana Chott, Tunisia katika ziwa la maji ya chumvi lililokauka. Hapa ndipo video ya nyumba ya Luke Skywalker katika filamu ya Star Wars ilichukuliwa.
VyooImage copyrightALAMY
Vyoo hivi katika eneo la Bahia, Brazil vimo katika kituo cha kutunza kasa.
Image copyrightALAMY
Choo hiki ambacho kinapatikana eneo lenye mandhari ya kupendeza kinapatikana Uswizi. Hapa ni mita 2,7000 katika milima ya Alps.
Image copyrightALAMY
Choo hiki katika duka la Standard Grill katika mtaa maarufu wa kufungia nyama New York kimeelezwa na wengi kama choo kinachokanganya ubongo.
Image copyrightALAMY
Vyoo hivi vijulikanavyo kama Between The Waters vinapatikana Emscherkunst nchini Ujerumani.
Image copyrightALAMY
Hapa ni Wellington, New Zealand. Kwa kutazama picha, ni vigumu kuelewa vyoo hivi hutumiwa vipi. Lakini waliozijenga walitaka zifanane na miguu ya kambakoche.

Friday, April 15, 2016

Mbwa wa Manchester watambua tamutamu pekee


WanyamaImage copyrightPA
Image captionMbwa hao waligundua tamutamu na nyara ya pori
Ripoti moja inasema kwamba mbwa wa kunusa katika uwanja wa Manchester Uingereza wamekosa kugundua mihadarati katika kipindi cha miezi saba.
Hata hivyo mbwa hao wanaweza kunusa tamu tamu kama vile jibini na soseji kutoka kwenye mikoba ya wageni wanaofika kwenye uwanja huo.
Mbwa hao sita wanaogharimu dola milioni mbili za Kimarekani kuwatunza walipata mafunzo ya kutambua mihadarati, tumbaku, pesa, nyama ya pori.
Hata hivyo kwa kipindi cha miezi saba maafisa wa uhamiaji wamesema walishindwa kupata dawa za kulevya aina ya kokeini na heroini.
Ripoti hii inapendekeza matumizi ya mbwa hao yabadilishwe.

Wednesday, April 13, 2016

Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka

Image captionPanya wailazimu Uingereza kukodisha paka
Je unampenda paka ?
Awe ni paka wa nyumbani ama yule paka wa mwituni na wanyama wote katika jamii ya pakaa kama vile simba,ama chui, paka huvutia hisia nyingi sana kwa mwanadamu.
Video za paka ni maarufu zaidi katika mitandao ya kijamii.
Image captionJe unampenda paka ?
Lakini mapenzi hayo ya paka yamefikia hatu mpya.
Amini usiamini afisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Image captionAfisi ya maswala ya nchi za kigeni ya Uingereza imekodisha paka ili kusaidia kudhibiti ongezeko la idadi ya panya katika makao makuu yake huko Westminster.
Paka huyo ambaye zamani alinusuriwa alipokuwa akizurura mitaani katika mji mkuu wa London -- alipewa jina Palmerston, jina la waziri mashuhuri wa zamani wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingereza na waziri mkuu karne ya kumi na tisa.
Kituo cha kuwanusuru wanyama, kimesema kwamba Palmerston, alikuwa mkakamavu na paka mwenye nguvu, ambaye haikuwa vigumu kwake kuwa na marafiki -- au maadui, katika makao hayo yake mapya katika afisi ya wizara ya nchi za kigeni.Panya wailazimu Uingereza kukodisha paka

Mtu mrefu duniani awasili Mauritius

Image captionSultan Kösen ana urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51.
Mtu mrefu zaidi duniani raia wa Uturuki Sultan Kösen aliye na urefu wa futi 8 na inchi 3 au mita 2.51 amewasilia nchini Mauritius leo asubuhi.
Sultan alilakiwa na umati katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye ukusara wa facebook wa mtandao wa habari wa nchi hiyo.
Image captionAliikinga kitabu Guinness World Records mwaka 2009.
Sultan mara ya kwanza alitajwa kuwa mtu mrefu zaidi duniani mwaka 2009 wakati alitimia urefu wa futi 8 na inchi moja mwaka 2009.
Akiongea wakati aliingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness World Records alismea," Singetarajia ningekuwa kwenye kitabu hicho, nikuwa na ndoto lakini bado ulikuwa ni mshangao mkubwa.Mtu mrefu duniani awasili Mauritius

Thursday, April 7, 2016

Mwanafunzi wa kiume anayepata ''hedhi''


Image captionGeorge na Amber May Ellis
George Fellowes ni mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 22 na anaamni kwamba hata yeye hupatwa na ''hedhi ya kiume''.
Anasema kuwa ni rafiki wa karibu wa Amber May Ellis jirani yake na hivyobasi hupata uchungu wa hedhi kila mwezi rafikiye anapopata hedhi.
Uchungu huo anasema huwa mkali hadi kulazimika kuchukua likizo ya kuwa mgonjwa.Akizungumza na Newsbeat,George anaelezea:Nadhani ni swala la kifikra kwa sababu sisi ni marafiki wa karibu sana na tuna hisia sawa.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliopita anasema kuwa amekuwa akipata uchungu wa hedhi na ishara hizo ni sawa na zile za wanawake.
Ninapata uchungu chini ya tumbo langu pamoja na katika kinena.Huwa nahisi vibaya na kuwa na hasira na marafiki wangu wengi.Pia huwa na hisia zenye mhemuko.
''Huwa sipendi kulia wakati huo lakini huwa na hasira nyingi.Kuna kitu kimoja kisichomuathiri George hatahivyo.
Sidhani kwamba wanaume wanaweza kupata hedhi bila kutokwa na damu'',anasema.
''Wakati unapokuwa rafiki wa karibu na mtu nadhani homoni zenu hufanana''.
Image captionGeorge na Amber May Ellis
George anaelezea kwamba wakati alipoanza kupata uchungu miaka mitatu iliopita alitaka ushauri wa daktari wake.
Lakini hakukuwa na maelezo hivyobasi alipewa dawa za kumaliza maumivu ya kinena.

Wednesday, April 6, 2016

Mamba mkubwa auawa Florida



LightseyImage copyrightLee Lightsey
Image captionLightsey alihitaji trekta kumbeba mamba huyo. Mamba huyo anaonekana hapa na mwanawe Lightsey, Mason
Mamba mkubwa mla ng’ombe ameuawa katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Mnyama huyo alikuwa na uzani wa kilo 360.
Mwindaji Lee Lightsey amesema mamba huyo wa ukubwa wa futi 15 (4.5m) ndiye mkubwa zaidi ambaye amekumbana naye katika kipindi cha miaka 18.
Baada ya kumuua, alihitaji trekta kumbeba.
Bw Lightsey alimgundua mnyama huyo akiwa na mwelekezi wa wawindaji Blake Godwin walipokuwa katika maeneo ya kumnyweshea mifugo maji Jumamosi.
Walimfyatulia risasi mamba huyo alipokuwa umbali wa mita sita kutoka kwao.
"Ingawa mnyama huyu ni mnene hivi, sijashangaa kwamba amekuwepo,” amesema Bw Lightsey.
“Tumewapata wengi ambao wamekuwa wadogo kiasi tu kumshinda katika miaka 20 ambayo tumekuwa tukiwinda.
"Kilichotuvutia ni kwamba anaonekana amekuwa akiwala ng’ombe wetu, kwa sababu tulipata vipande vya nyama majini. Alikuwa dubwana lililostahili kuangamizwa.”
Bw Lightsey anasema mamba mkubwa zaidi ambaye amewahi kumuua alikuwa na urefu wa futi 13ft (4m).
MambaImage copyrightGetty Images
Image captionMamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi pamoja kusini mwa Florida
Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja.
Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja.
Bw Lightsey amesema anapanga kumhifadhi mamba huyo lakini nyama yake ataikabidhi kwa wahisani.

Moyo wa nguruwe wapandikizwa kwa nyani


Image copyrightK H FUNGSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionUpandikizaji wa moyo wa nguruwe kwa nyani
Wanasayansi wanasema kuwa wameuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili.
Matokeo yake yanaweza kupiga jeki matumaini ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.
Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga.
Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu,kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin,kutoka kwa taasisi ya kitaifa ya Moyo ,Pafu na Damu huko Maryland,alikiambia chombo cha habari cha AFP.
Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.

Monday, April 4, 2016

Magari ya kifahari ya jeshi la Polisi Dubai, unakamatwa na kosa barabarani unasahau faini ukilishangaa gari


Dubai ni moja ya sehemu ukienda kwa mara ya kwanza utajikuta unashangaa tu tena kama wewe ni mpenzi wa magari makali na maisha mengine ya kifahari ndio kabisa maana kuanzia watu binafsi mpaka Jeshi la Polisi wanayo magari ya kifahari kamaFerrariBugatti na Lamborghini ambayo wengi wetu tumezoea kuyaona kwenye video za mastaa wa dunia kama kina Nicki MinajChris Brown na wengine.
Dubai ni moja ya sehemu chache duniani zenye usalama wa hali ya juu, mtaani hata iwe saa kumi au tisa usiku hakuna uhalifu na ninakumbuka mwaka 2014 nilifanya mahojiano na mwenyeji wa Dubai kwa zaidi ya miaka 20 akasema vitu kama wizi wa ukabaji au Majambazi hakuwahi kuvisikia, ishu alizowahi kuzisikia ni kama za visa vya mapenzi tu watu kupigana au kumletea mtu fujo sababu kakuchukulia mpenzi wako.
Kwenye hizi video hapa chini kuna Makala inayoonyesha Polisi wa Dubai wanavyofanya kazi na magari ya kifahari ya jeshi hilo ambayo yanaspidi kubwa kuliko magari ya kawaida lakini pia teknolojia waliyonayo kwenye kufatilia ishu za kiusalama.

HIZO HAPO JUU NI ZA POLISI, ZA RAIA MTAANI NI HIZI HAPA CHINI

Sunday, March 27, 2016

Tembea uone: hizi ni barabara nyingine 5 hatari duniani… utaendesha gari hapa?


BRNi dunia na ilivyoumbwa, kuna sehemu ambazo hatujawahi au hatutofika kabisa lakini teknolojia imeturahisishia na kutupa nafasi ya kuona kukojekukoje ambapo hii ya barabara nayo nilikua siijui, tazama list ya barabara zenyewe kwenye picha na hiyo video hapo chini baada ya picha.
BR 2
BR 3
BR 4
BR 5
BR 6
BR 7

Bumbuli ina miti hii ambayo Mizizi yake inaota kwenda Juu kama Ukuta..


Vipo vitu ambavyo ukivisikia unakua na maswali mengi sana kichwani,katika vitu ambavyo nimekutana navyo ni pamoja na hii ya Mizizi kuota kuelekea juu kama ukuta sio chini tena kama ambavyo tumezoea kwa mimea mingine.
5Mti huu unaitwa Entandrophragma Excelsum unapatikana kwenye Msitu wa Mazumbaiuliopo Bumbuli kwenye wilaya ya Lushoto kwenye mkoa wa Tanga na kizuri zaidi Msitu huu umehifadhiwa na Serikali chini ya chuo kikuu cha Sokoine kwa ajili ya watu kwenda kujifunza.
3Msitu huu wa Mazumbai nimewambiwa unasifa nyingi sana za kipekee,kwanza ni kati ya misitu michache ambayo haijaathiriwa na shughuli za kibinadamu na hii ni kutokana na ulinzi uliopo hapo pia msitu huu una aina nyingi za mimea kuliko aina za mimea inayopatikana Ulaya Magharibi.
2Waziri wa Nchi Ofisi Ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli Mh.January Makamba ni miongoni mwa Wageni waliopata nafasi ya kutembelea msitu huu.
1