Kuna watu tu wana mioyo ya kusaidia wengine na wameamua kufanya kwa vitendo, sasa baada ya kufanikiwa kuhudumia watoto zaidi ya 125 wenye vichwa vikubwa na migongo wazi huku watoto 55 wakiwa wamefanyiwa upasuaji, GSM Foundation na timu ya Madaktari bingwa kutoka MOI sasa wameingia Shinyanga.
Kuanzia kesho watakuwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga kutoa tiba bure kwa watoto kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea, kama una ndugu yako au yeyote mwenye Watoto wa aina hii inabidi waletwe kupata hii tiba bure ambayo imegharimiwa kwa asilimia 100% na GSM Foundation.
Watu zaidi ya 45
wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu visiwani
Zanzibar katika kipindi cha miezi miwili, shirika la habari la AP
limeripoti.
Shirika hilo la habari limemnukuu afisa wa afya visiwani humo anayesema vifo hivyo vimetokea mwezi Machin a Aprili.
Muhammed
Dahoma, ambaye ni mkurugenzi wa anayeangazia kuzuia maradhi katika
wizara ya afya, anasema watu karibu 3,000 wamelazwa hospitalini baada ya
kuugua.
Ameongeza kuwa serikali ya Zanzibar imechukua hatua kukabiliana na mlipuko huo.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupiga marufuku uuzaji wa chakula na juisi maeneo ya wazi.
Taarifa kutoka visiwani humo zinasema serikali pia imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana.
Waziri
wa elimu Riziki Pembe Juma, amenukuliwa na shirika la habari la Uchina
la Xinhua, akisema uamuzi huo umetolewa baada ya kubainika kwamba
wanafunzi ni miongoni mwa watu walioathiriwa zaidi na ugonjwa huo.
“Tumejaribu
kudhibiti hali, lakini kwa maslahi ya watoto wetu, watakuwa salama
zaidi wakisalia nyumbani,” amesema kupitia taarifa, kwa mujibu wa
Xinhua.
Ameongeza kuwa baadhi ya shule zimeathirika zaidi kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Kisiwa cha Unguja ndicho kilichoathirika zaidi ambapo watu 20 wamefariki na 400 kuambukiwa tangu Januari mwaka huu.
Waziri
wa afya Mahmoud Thabit Kombo aliambia gazeti la serikali la Daily News
wiki jana kwamba ikizingatiwa kwamba Zanzibar ni visiwa vidogo na watu
si wengi sana “kipindupindu sasa ni tishio kubwa”.
Mlipuko wa kipindupindu ulianza mwaka jana.
Kufikia Oktoba, visa 140 vya maambukizi vilikuwa vimeripotiwa katika visiwa hivyo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).