Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Muhuga akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati wa
uzinduzi wa kongamano la Vijana kuelelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana,
Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline
Castico akizungumza na Vijana na watendaji wa Mkoa wa Katavi (hawapo
katika picha) juu ya matumizi ya Tovuti ya Mkoa kabla ya kuzindua Tovuti
hiyo leo Mkoani Katavi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana,
Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline
Castico (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa Tovuti ya
Mkoa wakati wa kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi.
Baadhi ya Vijana wa Mkoa wa Katavi
wakifuatilia kwa makini mada zilizokua zikitolewa wakati wa kongamano la
vijana kuelekea uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo
Mkoani Katavi.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Katavi
Vijana Mkoani Katavi wametakiwa
kujitambua, kuchukua fursa na kuchangia maendeleo ya mkoa na taifa kwa
kutumia malighafi zinazopatikana mkoani humo kuwekeza na kuacha
kusubiria wawekezaji kutoka mikoa mingine ama nchi za nje kufaidika na
malighafi za mkoa huo.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe.
Jenista Mhagama alipokua akifungua kongamano la Vijana kuelekea uzinduzi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 leo Mkoani Katavi na kuwataka
vijana hao kuacha uvivu kwani maendeleo huletwa na jitihada za mtu
binafsi.
Mhe. Jenista amesema kuwa vijana
wanaweza wakajiwekeza katika sekta isiyo rasmi kwani sekta hiyo huajiri
asilimia kubwa na kuwagusa vijana wengi katika kutengeneza ajira na
kuwafanya vijana wasiwe tegemezi ndani ya jamii.
“Vijana wa Mkoa wa katavi mnayo kila
sababu kujitafiti na kujua ni namna gani mtatumia sekta isiyo rasmi
kutengeneza ajira ambazo zitawasaidia kuonyesha mchango wenu wa asilimia
55 kama vijana katika nchi ya tanzania ukaweza kutumika kuleta
maendeleo ya Mkoa na taifa kwani mnaweza, sababu mnayo, nguvu mnayo na
uwezo mnao” amesema Mhe. Jenista
Kwa upande wake Waziri wa Kazi,
Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Mhe. Moudline Castico amewataka vijana wa Mkoa wa Katavi
kutumia Tovuti ya Mkoa iliyozinduliwa wakati wa kongamano hilo kupata
taarifa kwa wakati ili waweze kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi
na teknolojia.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amesema kuwa Tovuti ya Mkoa yenye kikoa/domeini ya www.katavi.go.tzhttp://www.katavi.go.tz/
itakua na taarifa za uhakika na za wakati hivyo kuwawezesha wananchi wa
Mkoa wa Katavi wakiwemo vijana kujua taarifa za maendeleo za mkoa
pamoja na masuala mengine muhimu kama vile kuelimisha vijana masuala
muhimu ya kilimo bora, ujenzi wa viwanda vidogo na vikubwa, afya ya
jamii, taaluma za kibenki na ujuzi wa aina mbalimbali za kiteknolojia
utakaowawezesha vijana kujaribu.
No comments:
Post a Comment