Showing posts with label TAARIFA. Show all posts
Showing posts with label TAARIFA. Show all posts

Sunday, April 9, 2017

Breaking News: Msani Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa wapatikana Wakiwa Salama

Muda mfupi  baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro kuwaambia waandishi wa habari kuwa hawezi kusema ni lini mwanamuziki  Roma na wenzake watapatikana, taarifa kutoka kwa mmiliki wa studio walipokamatiwa, amethibitisha kuwa wamepatikana.

J Murder ambaye ndiye mmiliki wa Tongwe Records walipokuwa Roma na wenzake kabla ya kukamatwa na watu wasiojulikana, amesema kuwa wasanii hao wamepatikana na wapo katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Aidha,Mkuu wa polisi (OCD) wilaya ya Kinondoni, Abubakar Kunga amethibitisha kupatikana kwa wasanii hao, lakini kwa sasa amesema wanafanya nao mahojiano ya kipolisi katika kituo cha Oysterbay.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru.

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.
“Mimi ni Kamishna wa Polisi siwezi kusema wasanii watapatikana lini, kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana, muulizeni yeye.

“Upelelezi ndio utakao amua hawa watu watapatikana lini. Tunafanya kazi kufuata taaluma ni si kutoa maneno tu."
Alisema kamanda Sirro mapema Asubuhi wakati akiongea na waandishi wa habari

Saturday, January 21, 2017

Jeshi la Polisi lawaonya wananchi wanaofanya manunuzi kwa njia ya mitandao

Jeshi la polisi nchini limewataadharisha wafanyabiashara na wananchi wanaofanya manunuzi au kuuza bidhaa kwa njia za mtandao kuwa makini na matapeli wanaotumia mitandao kufanya uhalifu vikiwemo vitendo vya wizi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba na kutoa tahadhari hiyo kutokana na kuwepo kwa matukio mengi ya watu kuibiwa fedha zao wakati wa kuuza au kununua bidhaa kwa kutumia mitandao.
“Watu wamekuwa wakifanya biashara kwa njia za mtandao na matokeo yake wanajikuta wanaingia kwenye kutapeliwa kwenye kuibiwa kwasababu tu ametuma pesa kwa mtu ambaye hamfahamu, amefanya biashara na mtu ambaye hamfahamu yani wamewasiliana tu kupitia mtandao,” alisema Bulimba.
“Kwamba mimi nafanya biashara mbili tatu, mimi nauza kitu fulani nitumie pesa kiasi fulani ntakutumia mzigo, tunaomba wananchi wawe makini na hili suala kwasababu tumepokea matokeo mengi ya wananchi kutapeliwa kwa njia ya mtandao”.

Friday, May 13, 2016

Picha,Land Cruiser mpya ya mwaka 2016 ikotayari kuingia sokoni.

2e7c0c9a9af92e75a6122fb4b68318ad 21cde4ee4537761e2fee7b2b26d97826 bb9f836220e87380b382a01aa95b8496
VEHICLE TYPE: front-engine, 4-wheel-drive, 8-passenger, 4-door hatchback
PRICE AS TESTED: $85,199 (base price $84,820)
ENGINE TYPE: DOHC 32-valve V-8, aluminum block and heads, port fuel injection
Displacement: 346 cu in, 5663 cc
Power: 381 hp @ 5600 rpm
Torque: 401 lb-ft @ 3600 rpm
TRANSMISSION: 8-speed automatic with manual shifting mode
DIMENSIONS:
Wheelbase: 112.2 in
Length: 194.9 in
Width: 77.9 in Height: 74.0 in
Passenger volume: 141 cu ft
Cargo volume: 16 cu ft
Curb weight: 5926 lb
C/D TEST RESULTS:
Zero to 60 mph: 6.7 sec
Zero to 100 mph: 17.6 sec
Zero to 120 mph: 28.6 secRolling start, 5–60 mph: 7.1 sec
Top gear, 30–50 mph: 3.9 sec
Top gear, 50–70 mph: 5.1 sec
Standing ¼-mile: 15.1 sec @ 93 mph
Top speed (C/D est): 130 mph
Braking, 70–0 mph: 184 ft
Roadholding, 300-ft-dia skidpad*: 0.74 g

Saturday, April 30, 2016

Jipya kuhusu kifo cha Pamba Wemba, tazama huyu jamaa kwenye video

Taarifa  ambazo zinazidi kuenea kwenye vyombo vya habari Congo na mitandao ya kijamii hata hapa Tanzania ni msiba wa Papa Wemba lakini sasa mjadala umehamia kwenye namna kifo chake kilivyotokea
Kipande cha video kinachomuonesha jamaa akichukua mic halafu akairudisha kwenye stage na baada ya Pamba Wemba Kuanguka inadaiwa jamaa yuleyule badala ya kumsaidia alikimbilia mic ili isijulikane. Taarifa zinazoenea ni kwamba mic ile ilikuwa imewekewa sumu.
Hapa Mwanamuziki wa Congo anayeishi Tanzania, Papii Catalogue ameitafsiri video hiyo kwa lugha ya kiswahili, unaweza kuitazama……

Wednesday, April 6, 2016

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ateketea kwa Moto Akiwa Ndani ya Gari Lake


Mhadhiri  wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Kompyuta (CoICT), Dk Richard Mgaya amefariki baada ya kuteketea ndani ya gari lake jijini Dar es Salaam juzi.

Gari la Dk Mgaya liliteketea baada ya kugongana na lori katika eneo la Mbezi Africana, Wilaya ya Kinondoni usiku wa kuamkia juzi na kuwaka moto uliosababisha kifo chake.

Juzi picha mbalimbali zilisambaa zikionesha gari aina ya Toyota Prado lililopata ajali eneo hilo la Africana baada ya kugongana na lori, baadaye ilibainika kuwa aliyekuwa katika gari hilo ni Dk Mgaya.

Akizungumza  kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime alisema gari la Dk Mgaya liliteketea na hata kushindwa kujulikana dereva wa gari hilo.

Alisema baadaye ndugu wa marehemu ndio walithibitisha kuwa gari hilo lililoteketea na dereva aliyekuwemo ni Dk Mgaya ambaye hata hivyo naye aliteketea ndani ya gari hilo.

“Lile gari liliungua na hakuna kitu kilichopatikana, hata wakati polisi wanafika eneo la tukio walikuta tayari dereva amekuwa majivu kutokana na kuteketea kwa moto… labda baada ya kupima vinasaba ndio itathibitika kama ilikuwa ni yeye,” alisema Kamanda Fuime.

Alisema hata gari hilo hawakuweza kulitambua mara moja na baada ya kufuatilia Mamlaka ya Mapato (TRA) ilibainika kuwa mmiliki wake ni Dk Mgaya.

Alisema “ndugu wa marehemu ndio wamesema kuwa ni ndugu yao.” 

Dk Mgaya alijiunga na idara hiyo miaka kadhaa iliyopita akitokea masomoni nchini Marekani na alikuwa ni mtaalamu wa artificial intelligence.

Sunday, April 3, 2016



FAT PEOPLEUtafiti mpya umeonesha watu wazima wengi Duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene Duniani.

Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo cha Imperial cha London, wakiandika katika jarida la kimatibabu la Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene.

Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu.FAT PEOPLE11

Profesa Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna “mkurupuko wa unene”.

Wanasayansi hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya kuendeshea baiskeli.

Wanazihimiza serikali kuchukua hatua za pamoja, hasa kuhusu bei ya vyakula.Fat-People-Pictures-2

Baada ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba idadi ya watu wanene duniani imeongezeka kutoka 105 milioni mwaka 1975 hadi 641 milioni mwaka 2014.

Idadi ya watu walio na uzani wa chini ya kuwango imeongezeka kutoka 330 milioni hadi 462 milioni katika kipindi hicho.

Viwango vya unene miongoni mwa wanaume kilipanda kutoka 3.2% mwaka 1975 hadi 10.8%, na miongoni mwa wanawake viwango vya unene vilipanda kutoka 6.4 % mwaka 1975 hadi 14.9%.fat-people

Hii ina maana kulikuwa na wanaume wanene 266 milioni na wanawake wanene 375 milioni mwaka 2014.

Saturday, April 2, 2016

Mtu Mmoja Auawa Kwa Kuchomwa Kisu Jijini Mwanza Kisa Kikiwa ni Wivu wa Mapenzi




Mtu mmoja amefariki dunia, huku mwingine akijeruhiwa baada ya kuchomwa visu wakati wa ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi wilayani Ilemela mkoani Mwanza.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alimtaja aliyeuawa kuwa ni Makororo Kitota (26) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iloganzala, alichomwa kisu shingoni na kifuani na kupoteza maisha palepale.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu saa nne usiku katika kilabu ya pombe za kienyeji.

Kamugisha alisema mtuhumiwa aliyefanya tukio hilo alikuwa na ugonvi wa muda mrefu na Kitota akimdhania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe ambaye pia alikuwapo kilabuni hapo wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wametengana tangu Agosti 2015 kwa sababu hiyo hiyo kutokana na usaliti katika uhusiano wa kimapenzi.

Aliyejeruhiwa katika tukio hilo ni Nchama Wanda (33), mkazi wa Sabasaba wilayani humo aliyechomwa kisu tumboni na utumbo kutoka nje alipojaribu kuwaamulia wakati wakipigana.

Kamugisha alisema majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi na kwamba, hali yake siyo nzuri.

Alisema mke wa mtuhumiwa wa mauaji hayo anashikiliwa na polisi baada ya mtuhumiwa na mmiliki wa kilabu hiyo kukimbia kusikojulikana.

Kamanda huyo alisema jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watu hao ili kuwafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Monday, March 28, 2016

TAARIFA MPYA KUHUSU UJENZI WA BOMBA LA GESI


IMG_2077

Wizara ya Nishati na Madini Inaendesha mkutano na wafanyabiashara wa mafuta nchini ambao utalenga kuibua fursa zitakazo jitokeza katika mradi wa ujenzi wa bomba la Mafuta litakalo jengwa kuanzia HOIMA
nchini Uganda hadi bandari ya Jijini Tanga.

Akizungumza na wanahabari Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa amebainisha fursa zitakazojitokeza kupitia mradi huo kuwa ni pamoja na kupata tenda, ajira kwa vijana, kodi
itakusanywa kupitia mradi huo wa ujenzi.

“Mradi huo utapitia nchini lakini pia utaibua fursa mbalimbali zikiwemo ajira,tenda na utaongeza pato la Taifa kupitia ukusanyaji wa kodi”. Alisema
Katibu

Aidha Ntalikwa ameongeza kuwa ujenzi huo utaendeshwa kwa miezi thelathini na sita (36) na utaanza mara tu baada ya makubaliano baina ya Tanzania, Kenya na Uganda ambapo dalili zinaonesha wazi kuwa bomba litajengwa Tanzania kulingana na sifa ya nchi hiyo kuwa na Vigezo husika kama Uzoefu,Amani na Ulinzi.

Aliyeita mumewe ndovu apewa talaka India


NdovuImage copyrightThinkstock
Image captionMahakama imesema ni ukatili kumuita mume ndovu
Mahakama katika mji mkuu wa India imeamua kwamba ni kosa kwa mke kumuita mumewe “ndovu” na kosa hilo linaweza kuwa msingi wa talaka.
Mahakama Kuu mjini Delhi imedumisha uamuzi wa mahakama ya chini uliotolewa mwaka 2012 ambao uliidhinisha talaka.
Mahakama hiyo ilisema mtu kumuita mumewe ndovu ni “kumtendea ukatili wa kiakili”.
Mfanyabiashara aliyeitwa ndovu ana umri wa miaka 35 na alikuwa na uzani wa kilo 100.
Alisema mkewe alizoea kumuaibisha kwa kuwa mnene na "kutoweza kutimiza haja yake ya kimapenzi”, vyombo vya habari India vimeripoti.
"Hatua ya aliyekata rufaa kumbandika majina na kumrushia matusi mumewe kwa mfano kumuita 'Hathi' [ndovu], 'Mota Hathi' [ndovu mnene], hata kama alikuwa mnene bila shaka ingeathiri hadhi yake na kujiamini kwake,” Jaji Vipin Sanghi alinukuliwa na gazeti la India Today.
Mwanamke huyo alikuwa ameambia mahakama hiyo kwamba madai ya mumewe hayakuwa na msingi lakini mahakama haikukubaliana naye.

APP YA FACEBOOK HAITOTUMIKA KWENYE SIMU ZA BLACKBERRY


blackberry_phone_624x351_reutersUamuzi huo umesikitisha sana kampuni hiyo ya kutengeneza simu Blackberry.

Wanaotumia simu hizo za Blackberry watalazimika kutumia visakuzi vya kawaida iwapo wanataka kutumia mtandao huo wa kijamii kwenye simu zao.

Bado haijabainika hatua hiyo itatekelezwa lini

Mapema mwezi huu, WhatsApp, ambayo humilikiwa na Facebook, ilitangaza pia kwamba simu aina ya Priv za kampuni ya Blackberry.

Whatsapp itaacha kutumika katika mfumo wa simu za Blackberry kufikia mwisho wa mwaka 2016.

“Tulijaribu sana kushawishi WhatsApp na Facebook wabadilishe msimamo wao, lakini kwa sasa, uamuzi wao haujabadilika,” mtaalamu wa programu za simu wa Blackberry Lou Gazzola, aliandika kwenye blogu.

“Tumejibidiisha sana kutafuta njia ya kuwafaa wateja wetu na tunaendelea kutafuta suluhu mbadala.”

Bw Gazzola alitoa wito kwa wateja au watu wanaozipenda simu za Blackberry kutumia kitambulisha mada cha #ILoveBB10Apps (Nazipenda app za Blackberry 10) kulalamika.

Tanzania Yatajwa Kwenye Nchi 10 Zisizo na Furaha Duniani

Denmark imechukua nafasi ya Switzerland kama nchi yenye furaha zaidi duniani kwa mujibu wa ripoti iliyotoka Jumatano hii.

Ripoti hiyo imeandaliwa na ‘Sustainable Development Solutions Network and the Earth Institute’ katika chuo kikuu cha Columbia.
Ilionesha kuwa Syria, Afghanistan na nchi zingine 8 zilizopo chini ya jangwa la Sahara ndizo sehemu zisizo na furaha zaidi. Nchi hizo ni pamoja na Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda, Benin, Togo na Burundi.
Nchi 10 za juu zenye furaha zaidi ni Denmark, Switzerland, Iceland, Norway, Finland, Canada, Uholanzi, New Zealand, Australia na Sweden.
Nchi tano duniani, Bhutan, Ecuador, Scotland, UAE na Venezuela zimeteua mawaziri watakaoshughulikia ukuzaji wa furaha.
Tanzania tuna matatizo gani? Kuna umuhimu wa Magufuli kuanzisha wizara kama hiyo pia?