Jeshi la polisi nchini limewataadharisha wafanyabiashara na wananchi
wanaofanya manunuzi au kuuza bidhaa kwa njia za mtandao kuwa makini na
matapeli wanaotumia mitandao kufanya uhalifu vikiwemo vitendo vya wizi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu
Mwandamizi wa Polisi, Advera Bulimba na kutoa tahadhari hiyo kutokana na
kuwepo kwa matukio mengi ya watu kuibiwa fedha zao wakati wa kuuza au
kununua bidhaa kwa kutumia mitandao.
“Watu wamekuwa wakifanya biashara kwa njia za mtandao na matokeo yake
wanajikuta wanaingia kwenye kutapeliwa kwenye kuibiwa kwasababu tu
ametuma pesa kwa mtu ambaye hamfahamu, amefanya biashara na mtu ambaye
hamfahamu yani wamewasiliana tu kupitia mtandao,” alisema Bulimba.
“Kwamba mimi nafanya biashara mbili tatu, mimi nauza kitu fulani
nitumie pesa kiasi fulani ntakutumia mzigo, tunaomba wananchi wawe
makini na hili suala kwasababu tumepokea matokeo mengi ya wananchi
kutapeliwa kwa njia ya mtandao”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment