Msanii wa filamu, Dokii ameamua kufuata nyayo za Stereo kwa kuamua kumchana rapper Darassa kuwa anampenda.
Muigizaji amedai kwa sasa anamkubali sana Darassa kupitia kazi yake
ya muziki, lakini yuko tayari kuolewa naye endapo Darassa mwenyewe
atahitaji hilo.
“Nampenda sana Darassa, i love him, nampenda kwa sababu ya kazi yake,
lakini sijawahi kumwambia, he is handsome….Darassa mi nampenda kazi
yake but is very handsome, so what do you expect?… Mie sina mtu kwa
sasa, so kama Darassa akitaka kunioa, niko tayari, am ready coz he is
handsome” Dokii alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
Dokii alisema hayo ili kufafanua kuhusu picha ambayo ameonekana akiwa
amepiga na Darassa, picha iliyozua mjadala kutokana na kuwa katika pozi
lenye utata.
Pia alifafanua kuhusu mahusiano yake na msanii Rich Mavoko, ambapo alisema Rich ni ndugu yake hivyo hawawezi kuwa wapenzi.
Wiki chache zilizopita, rapper Stereo alimchana rapper Chemical kuwa anampenda na yupo tayari kwa lolote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment