Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri za serikali mojawapo
ikiwa ni agizo linalolenga kuifuta bima ya Afya iliyoanzishwa na
mtangulizi wake Barrack Obama maarufu kama Obamacare. Agizo hilo lenye
lengo la kuipunguzia serikali mzigo wa kiuchumi, linaziamuru taasisi za
kiserikali kukomesha hatua zitakazoendeleza bima hiyo inayofadhiliwa na
serikali. Badala yake linataka taasisi hizo kupunguza, kuchelewesha au
kufutilia mbali gharama za matibabu ambazo zilishughulikiwa na bima
hiyo. Hatua ambayo itaweka gharama hiyo kwa serikali za majimbo na watu
binafsi. Bima hiyo huwawezesha mamilioni ya wamarekani wasiojiweza
kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu. Kuiondoa kabisa bima hiyo
kutahitaji mswada kupitishwa katika bunge la Marekani
No comments:
Post a Comment