Saturday, April 30, 2016

BALOZI IDDI AKUNWA NA UJENZI WA DARAJA LA NYERERE


Watanzania watakiwa kutumia miundombinu inayojengwa na serikali kikamilifu ili ilete manufaa kwa taifa zima

Makamu wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi,  ametembelea daraja la Mwalimu Nyerere, Kigamboni, ambapo amewataka watanzania kuwa na imani na serikali yao kwenye miradi mbalimbali inayopangwa kutekelezwa na wahakikishe miradi hiyo wanaitumia katika kuwanufaisha.IDDIBalozi Iddi amesema kuwa kuna miradi mingi ambayo serikali imepanga kutekeleza ili kuhakikisha Tanzania bara na Tanzania visiwani zote kwa pamoja zinakuwa na maendelo sawa na kupelekea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakuwa nchi yenye uchumi wa kati.

Kwa upande wake meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja la Nyerere Eng.Karimu Mattaka amesema wamefunga mifumo maalum yakuchunguza shughuli mbalimbali zitakazokuwa zinafanyika katika mradi huo ili kuhakikisha wanaondoa masuala ya urasimu pindi mradi huo utakapoanza kukusanya mapato.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment