Saturday, April 30, 2016

MJADALA JUU YA MAFUTA YA UGANDA WAANZA


Waziri wa Nishati wa Uganda Bi. Irene Muloni pamoja na timu ya wataalamu wa wizara yake wapo nchini kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka nchini humo hadi jijini Tanga.

Bomba hilo litakalojengwa kwa ushirikiano baina ya serikali za Uganda na Tanzania, awali lilikuwa lipitie nchini Kenya na litakuwa likisafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la magharibi mwa Uganda mahali ambako imegundulika hazina kubwa ya nishati ya mafuta.

Mwenyeji wake, Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Profesa Sospeter Muhongo amewaambia waandishi wa habari  kuwa mbali ya bomba la mafuta, mkutano huo unaohusisha wataalamu kutoka nchi zote mbili, utajadili pia ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Tanzania kwenda nchini Uganda.muhongoKwa mujibu wa Profesa Muhongo, bomba la gesi litatumika pia kupeleka nishati hiyo katika mikoa ya kanda ya ziwa, kwa kutumia michoro na miundombinu itakayopita kwenye eneo lile lile ambako bomba la mafuta litajengwa.

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment