Polisi nchini Uturuki wamekamata mwandishi wa habari aliyemkosoa rais wa nchi hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Ebru Umar raia wa Uholanzi alikamatwa na polisi baada ya kumkosoa rais Recep Tayyip Erdogan alikamatwa katika mji wa wa magharibi wa Kusadasi jumamosi usiku.
Wizara ya maswala ya nje ya Uholanzi imethibitisha kuwa Bi Umar alichapisha ripoti iliyomkosoa Sera za rais Erdogan ya kuwataka watu wote wenye asili ya Uturuki kuripoti wakati wowote mtu anapomtusi au kumkosoa nchini Uholanzi.
Hapo jana rais wa baraza kuu la muungano wa ulaya Donald Tusk, aliitaka serikali iruhusu uhuru wa kujieleza kama inavyotakikana kikatiba itakelezwe.
Tusk ambaye alikuwa ameandamana na waziri mkuu Ahmet Davutoğlu alionya kuwa uhuru wa wanahabari unatishiwa na maamuzi ya wanasiasa wachache serikalini.
Bw Davutoğlu kwa upande wake ameamua kutetea rekodi ya Uturuki, kuhusiana na uhuru wa vyombo vya habari, katika kikao na waandishi habari kilichohudhuriwa na Bi Merkel na maafisa wakuu wa jumuia ya muungano wa bara Ulaya.
Rais wa baraza kuu la muungano wa jumuia ya EU Donald Tusk, alidokeza kuwa, wanasiasa wanafaa kuamua kuhusiana na swala la ukosoaji na uharibifu wa hadhi ya mtu, hasa kuhusiana na ukiukaji wa haki ya uhuru wa kujieleza kwa vyombo vya habari.
Baadhi ya wanahabari wa Uturuki wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kutoa siri za serikali.
Mwezi uliopita, gazeti kuu linaloandika maswala ya upinzani - Zaman, lilishuhudia wanachama wa halmashauri kuu ya usimamizi, wakifutwa kazi na mahala pao kujazwa na waandishi, wanaounga mkono serikali.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan pia, amekuwa akitathmini kuwasilisha mashtaka dhidi ya muigizaji wa kuchekesha, raia wa Ujerumani, ambaye alitoa matamshi ya kumkejeli.
No comments:
Post a Comment