Polisi katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wanasema kuwa takriban watu saba waliuawa wakati nyumba moja ilipoanguka katika mtaa mmoja mjini humo.
Waokoaji wanaendelea kutafuta watu wanaohofiwa kukwama ndani ya vifusi vya jengo hilo la ghorofa sita kufuatia mvua kali inayoendelea kunyesha ambayo imesababisha mafuriko.
Takriban watu 120 wameokolewa kufikia sasa katika mtaa huo wa Huruma.
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban familia 150 ziliathiriwa na mkasa wa jumba hilo lililojengwa miaka miwili iliopita
Waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Mama Lucy iliopo mjini humo.
No comments:
Post a Comment