Forbes wametaja list ya vijana 30 wajasiriamali kutoka nchi tofauti tofauti za Afrika, vijana ambao wanatazamiwa kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa kwa siku za usoni, list ya vijana hao 30 wanaotajwa kutoka sehemu mbalimbali Afrika wametajwa na kuelezewa historia zao za miradi yao midogo waliyoanza nayo.
Katika list ya vijana 30 wanaotajwa na Forbes na wanatarajiwa kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa kuna jina la mtanzania pekee ambaye Tanzania inapaswa kujivunia. Jina la Nadeem Juma ndio jina la mtanzania pekee lililotajwa kuwa katika list ya vijana hao 30.
Kama humfahamu Nadeem Juma ni mwenyekiti wa kampuni ya AIM Group. Nadeemni kijana wa Tanzania aliyeanza kufanyabiashara akiwa na umri wa miaka 19 kwa kuanzisha shule ya kimataifa ya Dar es Salaam International Academy (DIA).
Nadeem aliamua kuanzisha shule hiyo ya kimataifa baada ya kuona kuna ulazima waTanzania kuwa na shule itakayotoa elimu ya viwango vya kimataifa, kwani kwa kipindi hicho Tanzania kulikuwa hakuna shule za viwngo na asilimia kubwa wazazi wengi walikuwa wanalazimika kupeleka watoto wao Kenya, South Africa na Swaziland.
Haya ndio majina ya vijana wengine wa Afrika waliotajwa na Forbes katika list ya wajasiriamali 30
- Simbarashe Mhuriro, Zimbabwe
- Ntombenhle Khathwane, Swazi
- Olatorera Oniru, Nigerian
- Bonobo Ramokhele, South Africa
- Thato Kgatlhanye & Rea Ngwane, South Africa
- Lee Grant, South Africa
- Samuel Malinga, Uganda
- Vanessa Zommi, Cameroon
- Neo Ramaphakela, South Africa
- Mutoba Ngoma, Zambia
- Hilda Moraa, Kenya
- Eugene Mbugua, Kenya
- Jamie Pujara, Kenya
- Tyrone Moodley, South Africa
- Rachel Sibande, Malawi
- Mike Chilewe Jr, Malawi
- Kelvin Name, Rashad Seini na Kofi Amuasi, Ghana
- Ogunlana Olumide & Chukwuwezam Obanor, Nigeria
- Kasope Ladipo-Ajai, Nigeria
- Yasmine El Baggari, Morocco
- Aisha Ayensu, Ghana
- Anda Maqanda, South Africa
- Trushar Khetia, Kenya
- Abiola Olaniran, Nigeria
- Clarisse Iribagize, Rwanda
No comments:
Post a Comment