Friday, April 29, 2016

Colombia yahalalisha ndoa za mashoga



Colombia imekua nchi ya nne kuhalallisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja.
Colombia imekua nchi ya nne kuhalallisha ndoa kati ya watu wa jinsia moja.
Najet Benrabaa/RFI


Mahakama ya Katiba ya Colombia imehalalishwa Alhamisi ndoa kati ya watu wa jinsia moja. Nchi hii inakuwa ya nne katika Ukanda wa Amerika ya Kusini kuruhusu ndoa ya mashoga.

"Majaji wamethibitisha kwamba ndoa kati ya watu wa jinsia moja haikiuki utaratibu wa kikatiba wa sasa," Mkuu wa Mahakama ya Katiba Maria Victoria Calle amesema.
"Kila mtu yuko huru na anajitegemea kwa kuwa na familia (...) kwa mujibu wa hisia zao za kimapenzi na kuhudumiwa kwa kimatibabu sawa na kulindwa kama inavyoeleza Katiba na sheria," Victoria Calle ameongeza.
Mapema mwezi Aprili, Colombia ilichukuliwa hatua yenye maamuzi kwa kuhalalisha ndoa za mashoga, pamoja na kupitishwa kwa Mahakama ya Katiba, jambo lililokaribishwa kama la "kihistoria" na jumuiya ya mashoga.
Majaji sita kati ya tisa wa mahakama ya Katiba waliokutana katika kikao cha pamoja Aprili 7 walipiga kura dhidi ya ombi la jaji Jorge Pretelt, ambaye alipiga marufuku ndoa kati ya watu wa jinsia moja.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment