Thursday, April 21, 2016

UN yathibitisha, mamia ya wahajiri wameghariki pwani ya Libya


UN yathibitisha, mamia ya wahajiri wameghariki pwani ya Libya
Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa, mamia ya wahamiaji haramu wamezama katika maji ya pwani ya Libya baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama baharini.
Kamisheni ya Wakimbizi ya Umoja wa Mataifa imetangaza rasmi kwamba, wahajiri 41 tu kati ya 541 waliokuwa katika boti hiyo iliyozama karibu na mji wa Tobruk, ndio waliookoka. Hii ina maana kwamba, wahajiri 500 wamezama baharini.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa tukio hilo ndilo baya zaidi kuwahi kutokea baharini katika miaka ya hivi karibuni. Wahajiri hao kutoka nchi za Kiafika kama Somalia, Sudan, Ethiopia na Misri walikuwa wakitoroshwa kutoka katika mji wa Tobruk kuelekea Ulaya.
Manusura wa ajali hiyo wanasema walipanda boti wakiwa kati ya abiria 100 na 200 lakini walipofika baharini walichanganywa na wahajiri wengine na kuifanya idadi ya abiria wote kuwa zaidi ya watu 500.
Wakimbizi karibu laki mbili wameingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean katika mwaka huu pekee na wengine karibu 700 wamefariki dunia kwa kuzama baharini.
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment