Friday, April 29, 2016

Vijana wakutana New York kabla ya kongamano la 66 Korea Kusini yaanza


Vijana mustakhbali wao ni upi? Hawa ni vijana wa DRC huko Goma katika tamasha la amani. (Picha:MONUSCO / Abel Kavanagh)
Maandalizi ya kongamano la 66 la vijana litakalofanyika nchini Katika Jamhuri ya Korea Kusini, yameanza, na vijana wanakumbushwa kuhusu haja ya kulitumia kongamano hilo kama fursa ya kuchangia utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kitengo cha mawasiliano na umma, Maher Nasser, amesema kuwa amesema anatarajia kwamba kongamano la Korea Kusini mwezi ujao litatoa ajenda itakayojumuishwa katika mipango ya kutimiza malengo ya maendeleo endelevu.
Bwana Nasser amesema, ingawa si lazima kila kijana ayajue malengo yote 17 ya maendeleo endelevu, ni vyema waelewe yanahusu nini, kwani yanahusu watu, sayari dunia, ufanisi, ushirikiano, na amani.
"Tungependa kuwa na mustakhbali ambapo watoto wetu na wajukuu wetu wana fursa sawa na hata bora zaidi kuliko tulizokuwa nazo sisi. Lakini tukiendelea kwenye mkondo wa sasa wa kupuuza tunachofanya kuathiri mabadiliko ya tabianchi, rasilmali za sayari dunia na jinsi tunavyozitumia, kutumia ghasia kutatua migororo badala ya amani, hiyo itakuwa changamoto."
Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment