Image caption
Donald Trump
Mgombea kiti cha
urais nchini Marekani Donald Trump amepongeza hatua ya raia wa Uingereza
kujiondoa katika muungano wa Ulaya akisema "wamekomboa nchi yao".
Amesema hayo alipowasili Trump Turnberry kwa ufunguzi wa mgahawa wa Ayrshire na ukumbi wa gofu,baada ya kufanyiwa ukarabati.
Kuna madai kuwa alinunua Hoteli hiyo kwa kima cha pesa ambazo hazikutajwa mwaka 2014.
Ufungamano
wa kibiashara baina ya Scotland na bilionea huyo wa Marekani ulianza
muongo mmoja uliopita alipoahidi kudumisha urithi wa mamake Mary
MacLeod, aliyezaliwa Stornoway mwendo mfupi kutoka eneo la Hebrides.
Bwana
Trump ambaye anasifika kwa kumiliki hoteli nyingi za kifahari pamoja na
nyanja za gofu nchini Marekani pia alifungua moja ya Hoteli hizo nchini
Uingereza katika jimbo la Menie mjini Aberdeenshire,mwaka 2012 baada ya
mzozo juu ya mipango na masuala ya mazingira ambayo yalipingwa na
wenyeji waliokataa kuhama.
Maandamano dhidi mgombea huyo wa urais
wa Marekani wa chama cha Republican yanatarajiwa, kutoka kwa wale
wanaomlaumu kwa ubaguzi wa rangi.
No comments:
Post a Comment