Shambulizi katika Hoteli ya Naasa Hablood mjini Mogadishu Somalia 25 06 2016
REUTERS/Feisal Omar
Takriban watu 11 wameuawa jana
Jumamosi katika shambulizi kwenye hoteli ya mjini Mogadishu nchini
Somalia ambalo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab.
Shambulizi hilo ambalo ni la
karibuni katika mfululizo wa mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la Al
Shabab kulenga hoteli na migahawa, lilianza wakati mshambuliaji wa
kujitoa mhanga alipolipua bomu lililokuwa limetegwa garini nje ya jengo
la hoteli.
Watu wenye silaha walivamia hoteli iitwayo Naasa Hablood na milio ya risasi ilisikika kwa saa kadhaa, mashahidi wamesema, kabla ya mamlaka kutangaza mashambulizi kumalizika.
Vikosi maalum vya usalama vimekomesha shambulizi hilo baada ya kuwaua washambuliaji watatu ndani ya hoteli.
Msemaji wa wizara ya usalama Abdi Kamil Shukri, amewaambia waandishi wa habari kuwa raia kumi na mmoja, wawili kati yao madaktari, wameuawa katika shambulio hilo.

No comments:
Post a Comment