Serikali
ya Tanzania imepitisha bajeti ya shilingi trilion 29.5 kwa kupigiwa
kura huku wabunge wa upinzani wakiwa wametoka nje wakiwa wameziba midomo
yao kwa karatasi na plasta ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhika na
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson wakigomea vikao vya Bunge vinavyoongozwa
na Naibu Spika huyo
Katika
vikao vya Bunge la 11, wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakisusia
vikao hivyo kwa takribani siku 23 sasa kwa madai ya kutokubaliana na
ukandamizaji unaofanywa na Naibu Spika wa Bunge Dkt.Ackson Tulia.
Wakichangia
bajeti hiyo, Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mwijarubi
Muhongo pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage wamesema
bajeti hiyo inalenga kukuza uzalishaji.
Akijibu
hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Bajeti hiyo ikiwa ni
pamoja na ya kuongeza fedha katika ofisi ya mkaguzi wa serikali CAG ili
kutanua wigo wa ukaguzi pamoja na kuachana na mpango wa kuanza kuwakata
kodi wabunge katika mafao ya kiinua mgongo ya Wabunge, Waziri wa Fedha
na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema msimamo wa serikali upo pale
pale.
Kuhusiana
na makato ya kodi kwenye mafao ya wabunge, Dkt Mpango amesema kuwa
serikali imeamua kuwa itakata kodi hiyo kwa viongozi wote wa kisiasa
wakiwemo wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na
Rais pia, ili kuweka usawa katika makato ya kodi nchini.
Baadaye
jioni wabunge walipiga kura mmoja mmoja kupitisha bajeti hiyo, ambapo
wabunge wote 251 waliokuwemo bungeni walipitisha bajeti hiyo kwa kauli
moja, ambapo kila mbunge alijibu "Ndiyo" akimaanisha anaipitisha bajeti
hiyo.
Mapema
Asubuhi mara baada ya dua, wabunge wa upinzani waliziba midomo yao kwa
karatasi na Plasta na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge ikiwa ni ishara ya
kuonesha kutoridhika na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson.
Mbunge
wa Vunjo Kupitia chama cha NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia kwa niaba ya
wabunge hao alisema hawataacha kulalamikia ukiukwaji wa sheria
unaofanywa na kiti cha Naibu Spika.
No comments:
Post a Comment