Akizungumza na vyombo vya habari akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais Francois Hollande, Ban amesema anatarajia nchi za Ulaya zitaheshimu sheria za kimataifa na kuonyesha ubinadamu kwa makundi hayo yasiyo na hatia.
Akitolea mfano Katibu Mkuu amesema juma lililopita alitembelea kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki ambapo alikutana na kushuhudia madhila ya wakimbizi kutoka Syria, na Iraq.
Amesema wakimbizi hao ambao waliosafiri safari zisizo salama za muda mrefu ni wachovu na wanachotaka ni uslama na watoto wao, elimu na ajira ili waweze kushiriki katika maendeleo
No comments:
Post a Comment