Baharini kwa wote ni kauli mbiu inayotumika kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya mabaharia leo Juni 25, 2016.
Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linaadhimisha siku hii kwa mara
ya sita kwa kuangazia umuhimu wa mabaharia katika bahari duniani ambapo
Katibu Mkuu wa IOM Kitack Lim amekaririwa akisema mabaharia
hawatambuliwi huku wakitimiza jukumu muhimu la kuisongesha dunia.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika
ujumbe wa kuadhimisha siku hii amesema mabaharia wanalisha dunia,
huvalisha na kuihifadhi.
Ban amesema wana umuhimu katika kukuza uchumi jumuishi na aunaojali mazingira.
Sherehe za siku ya mabaharia zitafanyika rasmi Septemba 29 ambayo ni
siku ya kimataifa ya masuala ya bahari,ambapo umuhimu wa dhana hiyo
utamulikwa.
Sunday, June 26, 2016
Unknown
Web Developer
Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment