Takribani Waethiopia 19 wamekutwa wamekufa ndani ya lori nchini
Zambia baada ya kukosa hewa . Lori hilo linasadikiwa kuwa ni la mtandao
wa usafirishaji haramu wa binadamu na lilikuwa likielekea Afrika ya
Kusini.
Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , wahanga hao
walikutwa baada ya manusura kugongagonga kontena walimokuwa wakihitaji
msaada. Msemaji wa IOM Joel Millman amesema tukio hilo ni baya sana
kulishuhudia.
(SAUTI YA JOEL MILLMAN)
"Hili ni kubwakabisa tunalolifahamu, lakini kumekuwa na
visa vingine vya kutisha kwatika safari hizo siku za nyuma.Nadhani
ilikuwa mwaka jana au miwili iliyopita kulikuwa na tukio la wahamiaji
kuzama, ambao walishuhudiwa wakiliwa na mamba, lakini hatujawahi kuona
vifo vya kukosa hewa kwenye kontena kama hivi"
Kwa mujibu wa IOM manusura 76 waliojumuisha watoto, wamepelekwa kwenye makazi ya dharura.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment