Kamishna
Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova, ameliomba jeshi hilo kumpa
kitengo cha masoko ili aweze kulitangaza na kuliunganisha na wananchi,
ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maboresho ndani ya jeshi hilo katika
kukabiliana na uhalifu.
Kova alitoa ombi hilo jana mjini Moshi katika hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika Shule ya Polisi Moshi (MPA).
Alisema
jeshi hilo linaelekea kuzindua mpango wake wa matokeo makubwa sasa
(BRN) ,ambao unahitaji msukumo wa jamii katika kusaidia kukabiliana na
uhalifu wa aina mbalimbali ukiwamo wa mtandaoni na dawa ya kulevya.
Kova
alisema kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 40 kwa kushirikiana
na wastaafu wengine, wanaweza kusaidia na kuwa kiunganishi baina ya
polisi na raia kama njia bora ya kukabiliana na uhalifu kwa kutumia
kitengo cha masoko.
“Nimekuwa
mtumishi ndani ya polisi kwa miaka 40, ninaweza kutumika hata na Shule
ya Polisi Moshi kufundisha na hata kutoa uzoefu wangu ambao utalisaidia
jeshi katika kukabili uhalifu, kama mnavyoniona ninazo nguvu za kutosha
na ninalipenda Jeshi la Polisi,” alisema.
No comments:
Post a Comment