Wednesday, June 1, 2016

PLUIJM AENDA GHANA ‘KUONGEZA NGUVU’


KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans-van-der-Pluijm amendoka nchini kwenda Ghana mapumziko mafupi ya wiki moja.

Baadhi ya wachezaji wake kwa sasa wako na timu ya soka ya taifa ya Tanzania `Taifa Stars’ inayojiandaa kukipiga na Misri katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika Gabon mwakani.Hans-van-der-Pluijm

Pluijm aliyeondoka jana alisema ameona atumie muda huu mfupi wa mapumziko kutembelea familia yake na jamaa wanaoishi nchini humo, ambako ndiko alikozaliwa mke wake.

Alisema atatumia muda huo kuipumzisha akili na kutafakari namna ya kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika itakayoanza kutimua vumbi kuanzia Juni 17, mwaka huu siku ambayo Yanga itakuwa ugenini kucheza na Mo Bejaia ya Algeria.

“Niko safarini naelekea Ghana kwa mapumziko mafupi ya wiki moja, kusalimia ndugu, jamaa na marafiki. Nikirudi itabidi tuanze maandalizi makubwa ya kuhakikisha tunafanya vizuri katika mchezo ujao wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika,” alisema.

Hata hivyo, ilielezwa Pluijm huenda akatumia muda huo kuifuatilia timu ya Medeama ya huko ambayo imepangwa kundi moja na Yanga. Kocha huyo amewahi kuinoa Medeama.

Nyingine katika kundi hilo ni TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment