Mkazi
wa Dar es Salaam, Leornad Kyaruzi amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, kujibu shtaka la kutoa lugha ya kumdhalilisha Rais John
Magufuli.
Kyaruzi alifikishwa katika Mahakama hiyo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Magreth Bankika.
Akisoma
hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Wankyo Simon alidai
mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 2, mwaka huu katika jengo la
Tanzania Tower lililopo Barabara ya Sam Nujoma.
Mwendesha
mashtaka huyo alidai siku hiyo, mshtakiwa aliandika kupitia simu yake
ya mkononi ujumbe wenye lugha ya kumdhalilisha Rais Magufuli na kisha
kuusambaza kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp wakati akijua kuwa ni
kinyume cha sheria.
Mshtakiwa
alikana shtaka hilo na Hakimu Bankika alimtaka kuwa na mdhamimi mmoja
kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria ambaye atasaini dhamana ya Sh5
milioni na kufanikiwa kutimiza sharti hilo, hivyo kuachiwa kwa dhamana.
Awali,
upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakalika na
kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine. Hakimu Bankika aliahirisha
kesi hiyo hadi Julai 18, mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Wakati
huohuo, kitendo cha baadhi ya wadau kumchangia Issack Habakuki
aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais Magufuli mkoani Arusha,
kilitinga bungeni baada ya wabunge kuitaka Serikali kutoa maelezo ya
kina iwapo hakimdhalilishi kiongozi huyo wa juu nchini.
Mwongozi
huo uliombwa na Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia akimtaka Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe atolee ufafanuzi jambo hilo.
Mahakama
mkoani Arusha ilimtia hatiani kijana huyo mapema mwezi huu kwa
kumtukana Rais katika ukurasa wake wa Facebook na kumhukumu kulipa faini
ya Sh7 milioni au kwenda jela miaka mitatu na wiki iliyopita, wakazi wa
Arusha walimchangia Sh4.5 milioni kukamilisha faini hiyo.
No comments:
Post a Comment