Kama wewe ni mmoja kati ya watumiaji wa mitandao kwa kutumia smartphone yako, basi mtandao wa YouTube umetangaza maboresho katika application yao kwa watumiaji wa simu za mkononi.
YouTube wametangaza kuboresha application yao ya YouTube inayotumika katika smartphone, sasa unaweza kuweka video za YouTube
live streaming kupitia simu ya mkononi, unachotakiwa kufanya ni
kubonyeza button katika simu yako na video unayorekodi moja kwa moja
itaenda YouTube.
Maboresho hayo ya YouTube kwa application za simu za mkononi, unaweza ukaifananisha na ile application ya mtandao wa Periscope na itakuwa na option ya viewers kuweka comment zao kama kawaida. Mfumo huo wa live streaming kwa simu za mkononi wa YouTube unaitwa ‘YouTube Connect’
No comments:
Post a Comment