June 22 2016 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amehutubia katika Jubilei ya miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) iliyofanyika katika ukumbi wa Benki hiyo, mtaa wa Mirambo Jijini Dar es salaam.
Katika hotuba yake Rais Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda mfupi usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma kwa lengo la kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa…..
>>>’lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya haitazidi miezi miwili hatutaajiri mtumishi yeyote serikalini pia hatutatoa promosheni ili tufanye ukaguzi wote ili kusudi ndani ya serikali tuondoe hili tatizo la wafanyakazi hewa’
No comments:
Post a Comment